Friday, February 14, 2014

ROSE NDAUKA NUSURA AVULIWE NGUO NA KUNDI LA WATOTO AMBAO HAWAKUTARAJIA KUMUONA LIVE.

Rose Ndauka
Star wa filamu Swahiliwood Rose Ndauka amesema kuwa nusura avuliwe nguo na watoto hivi juzi kati katika sherehe ya kutimiza siku 40 za mwanae tangu azaliwe. Watoto hao walimvizia, kumvaa na kumng'ang'ania Rose baada ya kutotarajia kumuona uso kwa uso kwani siku zote wamezoea kumuona kwenye tv tu.

Akizungumza na Globalpublishers Rose ambaye amecheza filamu nyingi karibia na mastaa wenzake wote wakubwa nchini alisema "Hawakutegemea kuniona pale, wengi wamezoea kuniona kwenye TV. Daah nilipata wakati mgumu kidogo maana ilibaki kidogo wanivue nguo, lakini nashukuru Mungu niliwatuliza, wakanielewa nikarudi zangu ndani"



Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment