Sunday, February 9, 2014

BABY MADAHA HUJAROGWA BALI UMEJIROGA MWENYEWE: SHILOLE

Shilole
Baada ya Baby Madaha kusema kuwa nyimbo zake haziwezi kulinganishwa na za Shilole akidai kazi za Shilole hazina ubora hasimu wake huyo ameamua kumjibu. Akizungumza na mtandao mmoja Shilole amesema kuwa hawezi kupoteza muda wake kujibizana na Madaha anayesifika kuwasemea mbovumbovu wasanii wenzake kadhaa, Shilole alisema kuwa hana tatizo na Madaha na anamshangaa sana kupenda kumzungumzia ilihali yeye hana time naye.

"Ni kama Baby Madaha anavyonizungumizia mimi, mmekuwa mkiona na wengine mliumia mkasema sana kwanini ananizungumzia mimi, Baby Madaha sina tatizo naye lakini nashangaa amekuwa mtu wa kunizungumzia everyday i don't know why" alifunguka Shilole ambaye pia ni mzungumzaji mkubwa.

Shilole ambaye pia ni star wa filamu Swahiliwood kama ilivyo kwa Madaha aliendelea kwa kusema "wewe mwanamke mimi mwanamke mwenzio nafanya kazi , umeshawahi kuniona hata siku moja naenda kukuzungumzia somewhere? Muogope Mungu kukaa unamzungumia mtu ambaye hana time na wewe, hebu tubadilike wanawake tupendane tuache kuzungumziana vibaya"

Shilole ambaye amecheza filamu nyingi kuliko Baby Madaha alimalizia kwa kusema "kwani ukinizungumzia mimi vizuri utapata nini, najua kuna vitu vingi nimekuzidi lakini usikae kwa kunizungumzia vibaya, wanawake tupendane tupeane sapoti, ndiyo maana hatufiki mahali tunabaki tu kulalamika ooh nimerogwa..... hujarogwa umejiroga mwenyewe"

                                                         Baby Madaha
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment