Wastara |
1.Kwanza, katika filamu hii Wastara anaonekana kuwa tofauti na filamu zake zilizopita ukiangalia picha tu zinajieleza. Wastara anaonekana amecheza some bold scenes za kiuchokozi ambazo sio kawaida yake hivyo kumfanya awe mpya ana kusubiriwa kwa hamu.
2. Pili, filamu hata kabla ya kutoka imesababisha habari kuenea mitandaoni na magazetini kuwa Wastara na Bond ni wapenzi na wao kukanusha ingawa ukweli utabaki wanaujua wao wenyewe kama ni wapenzi kweli au lah! picha za filamu hii ambazo zilianza kusambaa kama promo ya filamu hiyo zilifanya watu waamini kuwa ni wapenzi kwa kuwa zilikuwa kimahaba zaidi kutokana na film yenyewe kuwa romantic but siku zote wenye akili wanajua kazi ya sanaa inahitaji uhalisia wa jambo flani linaloigizwa.
3.Tatu, kava la hili filamu linaonekana kuvutia hasa picha za Bond zilivyopigwa na kutoka vizuri ila sikupenda muonekano wa Wastara, usoni amepakwa mapoda mengi kama kamwagiwa unga...!!
4. Kingine ni kuwa Wastara ni muigizaji mwenye kipaji cha hali ya juu hivyo inatia hamu kutaka kuiona filamu hiyo ikitoka kama chemistry yake on screen itakuwa hot aidha akiwa na Bond au Stanley Msungu. Inatia hamu kujua hivyo hasa baada ya habari kusambaa kuwa yeye na Bond ni wapenzi ingawa wenyewe walishakanusha.
5.Stanley Msungu mara nyingi hufanya vizuri kwenye nafasi zake anazopangiwa kuigiza so inatia bashasha ya kutaka kuona amefanya nini tena katika Uaminifu Dhaifu.
6. Mwisho kuona zaidi uwezo wa Bond kama director ambapo tayari ameanza kuwapa changamoto waongozaji waliomtangulia kwenye fani baada ya kutwaa tuzo ZIFF.
No comments:
Post a Comment