|
Sabby akisaini mkataba |
Licha ya kwamba hana muda mrefu hata mwaka haujaisha tangu aanze kuigiza filamu, Salma Tamim maarufu kama Sabby Angel tayari amesainishwa mkataba na kampuni ya Steps Entertainment Tanzania ambayo hujishughulisha na usambazaji wa filamu Swahiliwood. Habari za uhakika ni kuwa Sabby aliyejaaliwa mvuto wa haja amesainishwa mkataba huo awe ana-produce filamu zake mwenyewe baada ya filamu zake kuanza kutoka na kufanya vizuri sokoni licha ya kuwa newcomer hivyo Steps kuingia nae mkataba haraka. Licha ya mkataba huo wa kumtaka wa kutengeneza filamu zake mwenyewe ambazo zitasambazwa na Steps lakini bado anaruhusiwa kucheza filamu za watu wengine hasa zinazosambazwa na kampuni hiyo.
Hii ni kama bahati ya mtende kwa muigizaji huyo kwani wapo waigizaji wa siku nyingi ambao wanasota kila siku wapate mikataba ya filamu lakini bado inakuwa ngumu kwao. Hii inaonyesha kuwa Sabby ameanza kufanya vizuri sokoni ndiyo maana kampuni hiyo ikaingia nae mkataba. Angalia picha exclusive hapo chini Sabby akisaini mkataba na Steps...........
Follow us on twitter Swahili World Planet and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP
for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities,
features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and
Nollywood news, life styles news and more
No comments:
Post a Comment