Friday, January 17, 2014

NACHEZA FILAMU ZENYE MAADILI TU: SALLAI MAJASIRI.

Sallai Fatakid
Sallai Majasiri ni mmoja wa wasanii wa Afrika mashariki na kati wanaoishi Ulaya yeye akiwa Holland ambapo ana asili ya Congo lakini akiwa amekaa sana nchini Tanzania kabla ya kwenda Holland ambako anaishi na mkewe na watoto wake 3. Hata hivyo Sallai yeye anafanya zaidi music na filamu za gospel tofauti na wasanii wengi ambao hufanya sanaa za kidunia zaidi. Swahiliworldplanet ilipata nafasi ya kumuuliza machache kuhusiana na kazi na maisha yake binafsi hivyo soma hapo chini mjue zaidi msanii huyu..

SW: Unayaonaje mazingira ya Holland na Scandinavia kwa ujumla kisanii hasa kwa waafrika na filamu za kiswahili?

SALLAI:  Mazingira ya kisanii hapa Holland na Scandinavia kwa sasa ni ngumu kiasi maana ndio kwanza tunaanza ... Lakini inatia moyo mno na kuonesha kuwa huko mbele ,Mungu akitujalia kuna mafanikio makubwa kwa filamu na kazi nyingi za kiswahili ...

 SW: .Kwanini umeacha kuimba Gospel na kuamua kuanza kuigiza movies za Gospel?

SALLAI:  Sijaacha kuimba Gospel , bali nafanya vyote . Naigiza kwa kuhubiri kile nilichokitaka kukiimba kwa muziki , pia napo pata nafasi ya kuimba , naimba pi.

SW:  Wasanii wa Gospel na sanaa za kiburudani huko unawaonaje katika kazi zao na kwa mashabiki?

SALLAI:  ....Wasanii wa Gospel huku ,tunahitaji mno kua karibu na Mungu kuliko hata Africa . Maana hapa Ulaya na hata Amerika , Australia kuna shughuli nyingi mno zinazo weza kukuweka mbali kabisa na maombi na hata desturi ya mkristo wa kweli . Kwa kifupi huku roho wa Mungu iko mbali kiasi , ukilinganisha na roho za uovu , kwa maana kwamba mengi hapa hayampi MUNGU muumba utukufu . Kuna uhuru wa kiibilisi , kwa wote vijana ,watoto ,wanandoa ...Huku usipo kuwa makini na mtulivu kiroho na asiye na pupa na anae puuza mambo mengi ya kisasa ,unaweza kula hasara ya nafsi yako na wapendwa wako milele ni hasara mbaya kuliko unavyodhani !!! Mashabiki wapo lakini wamejigawa mno kimatabaka ... Maisha ya huku ni ya ndani mno siyo rahisi kuwafikia wengi kwetu watu wa gospel ya YESU KRISTO . Lakini wasanii wenzetu wasiofanya gospel wanaweza kufanya vyema kuliko maana watu wengi upenda sherehe na dansi na kujichanganya kuchangia kilevi...

SW:  Kazi zako za Gospel unauza mpaka nchi za Afrika au ni huko huko Scandinavia pekee?

SALLAI:  Bado sijaanza kuuza kazi zangu , maana nilikua sijatulia sana ki makao . Lakini zilifanya vyema Radio Praise power Tanzania na Kenya , Burundi...
Sallai akiwa na Selembe Toko

SW:  Je umeoa na una watoto wangapi?

SALLAI:  Nimeoa na nina watoto wa tatu , na sote tunaishi hapa Holland.

SW:  Umesema wewe ni mkongo lakini kiswahili chako ni kizuri je ulianza kukaa Ulaya mwaka gani?

 SALLAI:  Mimi ni mkongomani ambae natokea Kongo ya mashariki ambapo tunaongea kiswahili fasaha... Nilifika hapa Ulaya mwaka 2011 mwishoni . Nilikaa Dar es salaam maeneo ya Sinza halafu nikaelekea Kenya na huku (Holland) nikaja mwaka juzi(2011).

SW: Msanii gani wa injili kutoka Tanzania na Afrika kwa ujumla wakubali sana kazi zake?

SALLAI:  Nawakubali wote wanaofanya kazi ya MUNGU kwa utukufu wa MUNGU kwanza ,wasiojikweza ama kubabaika na pesa amaumaarufu , nawakubali walio sababu ya ya wengi kuja kwa YESU .

SW:  Umetoa album yoyote mpaka sasa ya muziki wa injili au na filamu ambazo sio za gospel unacheza pia?

SALLAI:  Niko na albam yangu ambayo sijaitoa , bali kuna singo kadhaa zilipigwa pigwa Tanzania ,Kenya na Burundi na mashariki mwa Congo. Niko na filamu ambayo iko tayari kwasasa ,MWANZO WA MWISHO lakini nimekataa kuiachia , na sina mpango tena wa kuiachia , nimeona ni bora niigize upya kabisa ama nije na nyingine, ni kwasababu maalumu kabisa ingawaje nilishaitangaza sana pia ahadi iko palepale kuwa haitouzwa , na basi kama sikuitoa , basi itakuwa ni nyingine kwa ahadi hii ...Nacheza filamu zilizo na maadili pekee ndizo ninazoweza kushiriki tu , hata kama siyo ya injli lakini ikiwa na maadili mema katika jamii nitaigiz.

SW: Ungependa kuwaambia nini mashabiki wa kazi zako?

SALLAI:  Nina maneno kibao simchezo!!. Lakini labda ningependa kuongeza kuwa ninafanya kazi na mdogo wangu anayeitwa Gilbert Fataki kwenye kampuni yetu ndogo ya kuandaa filamu #MAJASIRI PRO. na nina mpango wa kuja na filamu mpya kwa jina la JIPU KANISANI itakayofungua ukurasa mpya kwenye filamu za kiswahili kote haswa makanisani. Nitashirikiana na wasani wazoefu wanaongea Kiswahili wanaoishi hapa Ulaya . Akiwamo Selembe Toko , Rose almaarufu kama Devotha Alfred, Ashley Toto ,Gilbert Fataki na wengine wengi ambao sijawataja hapa ... Wazazi na wapenda maadili mema watarajie mambo mazuri katika kila filamu yangu.SALLAI MAJASIRI.

Pia ningependa kumalizia kwa kusema, ile short film ambayo tulicheza na Selembe , Gilbert na mimi . Ni chini ya V.A.D production & Majasiri Pro . Kwahiyo shukurani zangu za dhati kabisa kwa uongozi mzima na wana-VAD wote kwa ujumla , shukurani za dhati kwa director wa VAD JAY .

Bonyeza hapa ili kuona moja ya kazi za Sallai Gospel
Sallai akiwa na wenzake



 
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment