Kwanza ni Wema kutumia sana kiingereza ilihali wafuatiliaji au mashabiki wake wengi ni watu wa kawaida Tanzania ambao wengi hawajui kiingereza na yeye kwenye show yake ameonekana kuzungumza sana kiingereza. Inawezekana pia amewa-target mashabiki wake wa nchi nyingine za Africa mashariki ambao hawajui kiswahili vizuri lakini anatakiwa ajue kuwa asilimia kubwa ya mashabiki wake wapo Tanzania. Hivyo basi wawe wanatafsiri pia chini kama akizungumza english basi waweke tafsiri chini ya kiswahili na kinyume chake huku akipunguza kidogo matumizi makubwa ya kiingereza. Nimeifuatilia show hiyo tangu ilipoanza lakini mara zote ninapotazama na watu wengine ambao ni mashabiki wake wanaonekana kutoipatiliza wakidai kajaa uzungu mwingi na wao hawaelewi vizuri anachosema tena wengine ni wa kina mama wa nyumbani na sio vijana ambao ndiyo mashabiki wake wengi.
Pili ili "In My Shoes" ipate umaarufu zaidi nje ya nchi na kuwa na wafuatiliaji wengi Wema anatakiwa aendelee kucheza filamu kama mwanzo hii ni kwa kuwa watu wengi wa nje watakuwa wanamuona katika filamu na kujua ni star wa filamu Tanzania hivyo ni rahisi kufuatilia show yake kuliko ilivyo sasa umaarufu wake upo zaidi Tanzania sababu ya kuandikwa sana kwa skendo zake na maisha binafsi na magazeti ya udaku lakini filamu akiwa hana mpya sokoni kwa kipindi kirefu. Hakuna shaka kuwa wapo waigizaji wa Tanzania wengi wanaojulikana sana nje ya nchi kuliko Wema Sepetu kwa kuwa mastaa hao kama Jackline Wolper, Lulu, Irene Uwoya, Rose Ndauka, Riyama, ,Monalisa na wengineo wamecheza filamu nyingi ambazo zinauzwa nchi mbalimbali za Afrika mashariki, kati na zaidi hivyo kuwafanya wajulikane sana nje. Wema ana umaarufu mkubwa Tanzania na ushawishi pia lakini kwa nje hajulikano sana. Mfano kuna baadhi ya wakenya na watu kutoka burundi waliwahi kuniuliza "huyu Wema Sepetu ni nani mbona mnamuandika sana kwenye mitandao lakini filamu zake hatuzioni huku tunaona za kina Wolper, Irene Uwoya na Ray na JB?.
Inajulikana wazi kuwa Wema hapewi nafasi katika filamu kwasasa kwa kuwa anataka pesa nyingi ambazo ma-producer hawawezi kumlipa kutokana na soko la filamu kutokuwa la uhakika huku producers wenyewe wakilalamikia kila siku kunyonywa na wasambazaji. Lakini Wema kupitia kampuni yake anao uwezo wa kutengeneza filamu na zikauzika sana tu na kujiingizia faida kubwa kuliko hata akicheza filamu za watu kwani jina na sura yake vinauza hata filamu ikiwa mbovu. Ila kuna habari kuwa kutokuwa na upeo katika tasnia ya filamu kwa baadhi ya wafanyakazi wake ndiyo sababu ya kampuni yake kuwa kimya mpaka sasa mwaka unaisha bila kuwa na filamu sokoni licha ya kampuni hiyo kutabiriwa kuleta ushindani mkubwa wakati inazinduliwa mapema mwaka huu lakini imekuwa kimya mpaka sasa huku Kajala ambaye alidaiwa kusainishwa na kampuni ya Wema nae akiwa hana nguvu bado katika filamu.
Wema na team yake kama wakijipanga vizuri anao uwezo wa kusambaza kazi zake za filamu na hata za wasanii wenzake na kuleta ushindani mkubwa kwa wasambazaji wa sasa. Lakini filamu yake ya Superstar mpaka sasa haijulikani ilipo takribani mwaka na nusu sasa tangu itengenezwe licha ya kutumia pesa nyingi. Wema anatakiwa ajue kuwa hii ni Tanzania, Afrika mashariki na Afrika hivyo asidhani kuwa show yake itakuwa na umaarufu kama ule wa Keeping Up With The Kardashians ambayo ipo ulimwengu mwingine ikisapotiwa na media za kimataifa kupitia kwa star wake Kim Kardashian. kwasasa magazeti ya udaku ndiyo yanamuweka juu Wema maana Miss Tanzania tayari ilishapita zamani na uwepo wake kwenye tasnia ya filamu unapotea hivyo kama asipochanga vizuri karata zake mapema kujiimarisha katika tasnia ya filamu basi magazeti ya udaku yatakapoamua kumpotezea kama baadhi ya waigizaji wenzake ni rahisi kushuka kiumaarufu haraka hata kama akiwa na pesa. Kuna mastaa wenzake wengi tu ambao umaarufu wao ni wa kazi za filamu na sio skendo na wala huwa hawaandikwi magazetini. Akijiimarisha sasa katika filamu atazidi kujipatia umaarufu nchi nyingi za kiafrika na show yake itakuwa rahisi kuvuta vituo vingine vya Tv kufanya na e kazi.
No comments:
Post a Comment