Diamond Platinumz amefunguka kuwa kwenye maisha yake ya
ndoa atakayoingia siku chache zijazo, aliyekuwa mchumba wake wakamwagana
na kurejeana hivi karibuni, Wema Sepetu asitegemee kuolewa naye.
Diamond ambaye ni staa
wa Bongo Fleva aliyasema hayo mbele ya Globalpublishers kufuatia kuulizwa anamchagua nani wa kumuoa kati ya Wema
Sepetu na mchumba wake wa sasa, Penniel Mungilwa ‘Penny’.
Swali kwa Diamond
liliibuka baada ya kuzagaa kwa tetesi kwenye mitandao ya kijamii kwamba
yupo mbioni kumvisha pete ya uchumba mmoja wa mademu zake.
Swali hilo lilimfanya
Diamond afunguke kwa kusema kwamba anachokijua yeye na ambacho kipo
kwenye mikakati yake, mke wake mtarajiwa ni Penny.
“Najua wengi wanahisi
mimi ninaweza kuoa mwanamke zaidi ya mmoja kutokana na dini yangu
kuruhusu lakini jambo hilo mimi silifikirii hata kidogo kwa kuwa kwenye
maisha yangu nilishapanga nitaoa mke mmoja tu,” alisema Diamond.
Akaendelea: “Watu
wanasema mengi juu yangu na Wema, wengi wao hawajui nafsi yangu inataka
mwanamke yupi, ninachoweza kusema na watu wakasikia na kunielewa basi
wajue kwamba Penny ndiye mke wangu, Wema asitegemee kuolewa na mimi"
Diamond alikwenda
mbele zaidi kwa kumwanika Penny kwamba ana sifa ya kuwa mke kwani ni
mvumilivu sana na anaonesha upendo wa dhati kwake.
“Kwa maana hii basi
hakuna mwanamke mwenye jina kubwa wala sura nzuri zaidi ya Penny
ninayeweza kumwita mke wangu. Najua kila mtu ana namna yake ya kuchagua
ampendaye, ndiyo maana utaona watu wanasema hili mara lile, lakini
hawajui nafsi yangu inataka mwanamke wa aina gani,” alisema Diamond na
kuongeza:
Kama kuna demu
anayejipa matumaini hayo basi asitegemee hata siku moja kwa sababu kuoa
kwangu kutazingatia mke mwema na si bora mke, Penny pekee ndiye mwenye
sifa za kuwa mke wangu,” alisema Diamond.
Diamond na Wema Sepetu................
No comments:
Post a Comment