Wednesday, November 13, 2013

MTOTO WA LUCY KOMBA KUFUATA NYAYO ZA MAMA YAKE KATIKA TASNIA YA FILAMU.

Waswahili wanasema kuwa "mtoto wa nyoka ni nyoka" kauli hii inaweza kudhihirishwa na Lucy Komba na mwanae wa kumzaa Stromson ambaye ni mdogo tu mwenye miaka kama 4 lakini tayari akionyesha dalili zote za kuwa muigizaji mzuri hapo baadaye. Swahiliworldplanet ilimshuhudia live mtoto huyo juzi kati akiwa na mama yake huku akionyesha uchangamfu mkubwa, kuimba na pia kuonyesha vituko na kipaji cha uigizaji. Kwa ufupi mtoto wa Lucy Komba tayari amerithi kipaji kutoka kwa mama yake na katika zile filamu za watoto hasa characters za watoto watukutu au role za comedy anacheza vizuri bila wasiwasi na kuuvaa uhusika vizuri.

Lucy Komba alipododoswa na .Swahiliworldplanet kuhusu kipaji cha mwanae huyo alisema ni kweli ana kipaji na tayari kuna filamu kamchezesha lakini pia anataka mwanae apate elimu ya kutosha kwanza na sanaa ifuate.

Angalia picha za mtoto huyo..........................
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment