Thursday, November 21, 2013

LOVE MANIAC: CHUCHU HANS AWA KICHAA BAADA YA KUANGUKIA KATIKA PENZI LA RAY NA KUMTOSA WALTER.

Chuchu Hans
RJ Company chini ya Blandina Chagula(Johari) na Vicent Kigosi(Ray) wanakuja na filamu mpya ya Love Maniac na hii ni exclusive news ambayo Swahiliworldplanet imeipata kutoka kwa chanzo makini kilicho karibu na watengenezaji wa filamu hiyo. Kama hivi karibuni umeona Ray akiwa na tattoo nyingi mwilini na nywele za blond basi ni kwa ajili ya character yake katika filamu hii ambapo amecheza kama kijana wa kisasa na mhuni. Muigizaji mkuu wa kike wa filamu hii ni Chuchu Hans ambaye anapendwa sana kimapenzi na kijana mstaarabu ambapo nafasi hiyo imechezwa na Walter De Ngonde lakini Chuchu hapendi wanaume na hamtaki kabisa Walter ambaye anafikia hatua anawatumia wazazi wake(Mzee Masinde) wamsaidie kumpata Chuchu lakini mwishowe Chuchu anaangukia kimapenzi kwa kijana mhuni mwenye tattoo nyingi mwilini ambapo nafasi hiyo imechezwa na na Ray na hatimaye Chuchu anakuwa kichaaa kutokana na issues za mapenzi. Mastaa wengine katika filamu hiyo ambayo bado inashutiwa kwasasa ni Kupa.

                                             Walter De Ngonde

Muonekano wa Ray katika filamu ya Love Maniac......
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment