Tuesday, November 12, 2013

IRENE UWOYA AANZA MAZOEZI YA KUPUNGUZA UZITO BAADA YA KUDAIWA KAJIACHIA SANA NA KUPOTEZA MVUTO WAKE.

Irene Uwoya ameamua kuanza mazoezi ya kupunguza unene na kujiweka fiti na kurudisha mvuto wake wa awali ambao unadaiwa kupotea mara baada ya kujifungua huku media na wataalamu wa fashion wakimuandama mara kwa mara kuwa kapoteza mvuto wa mwanzo kwa kujiachia kunenepeana kiasi cha kupoteza mvuto. Owoya yupo chini ya mwalimu wake wa mazoezi Rashid Matumla ambaye ni bondia maarufu nchini na pia wanakuja na filamu wakiwa pamoja ambayo inaitwa Raundi Ya 8.
akizungumza na Filamucentral "Nimejipanga kwa kufanya mazoezi ya nguvu chini ya mwalimu wangu Rashid Matumla na nipo fiti kwa ajili ya kujifua najua kuigiza ndio ajira yangu lakini nikijiachia na kunenepa bila mpango nitaanza kucheza nafasi za akina bibi muda si mrefu na najiona mwili
unavyoninyemelea sitaki manyama uzembe"

 Filamu hiyo imeshutiwa Tanga, Dar es salaam na Morogoro huku waigizaji wengine wakiwa ni Francis Cheka na Lumolwe Matovolwa.

Uwoya akiwa na Rashid Matumla....................
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment