Thursday, November 28, 2013

ALI KIBA NDIYE ALIYENIFUNDISHA MAPENZI, NILIMPENDA SANA JUX: JACKLINE WOLPER

Jackline Wolper
Jackline Wolper ambaye ni star mkubwa wa filamu Swahiliwood kwa mara ya kwanza amekubali kuwataja wapenzi wake wa zamani na pia kuelezea kwa kirefu uhusiano wake na aliyewahi kuwa mpenzi wake kipindi cha nyuma Dallas. Katika interview na Globalpublishers Wolper ambaye pia ni actress anayelipwa pesa nyingi nchini alisema kuwa uhusiano wake na Dallas ulifikia kikomo kwa kuwa alikuwa na wanawake wengi na alikuwa haeleweki. Vile vile star huyo alisema kuwa Ali Kiba ambaye ni star wa muziki wa Bongofleva nchini ndiye aliyemfundisha mapenzi kwa mara ya kwanza kabla hata wote hawajawa mastaa lakini Kiba alipochomoka kimuziki na kuwa star aliamua kuachana nae baada ya kusikia kuwa mademu wanamshobokea sana.

"ni kitambo kidogo wote hatukuwa mastaa lakini yeye alifanikiwa kuchomoka, kabla ya Ali(Kiba) nilikuwa na mwanaume lakini hatukuduu kwa maana ya utu uzima ilikuwa yale ya kitoto, lakini Ali ndiye hasa aliyeniingiza kwenye ulimwengu wa mapenzi" alisema Wolper. Aliongeza kwa kusema "Ali akawa star alipokwenda nje nikasikia wanawake wanamshobokea, sasa mimi sikutaka karaha nikakaa pembeni lakini jamaa ni mtu poa sana na tukikutana tunasalimiana fresh kabisa"

Wolper alikiri pia kuwahi kuwa katika penzi na Diamond Platinumz ila walidumu kwa kipindi cha mwezi mmoja tu na pia alisema walikuwa ni washirika wa kibiashara ambayo hakuitaja. Katika list hiyo ya wapenzi wake wa zamani yupo Jux ambaye ni msanii wa Bongofleva pia yupo. Wolper alisema kuwa alikuwa na Jux kabla ya Dallas na mwanume aliyekuwa nae wakati wa Dallas na alimpenda sana Jux kwa kuwa ni mtafutaji. "Jux nilikuwa nae kabla ya Dallas na yule mwanaume wangu niliyeachana nae wakati wa Dallas, katika maisha yangu nilimpenda sana Jux, siyo marioo ni mwanaume mtafutaji aliyejiamini, kwasasa sipo naye, Dallas alichangia pia mimi kuachana na Jux" alisema Wolper ambaye kwasasa ana mwanaume mwingine.

                                                                Jux

Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment