Irene Uwoya anadaiwa kujihami na baadhi ya magazeti yanayotaka kumharibia katika kazi zake za filamu kwa kumshusha kwa nguvu alipo sasa bila sababu za msingi. Chanzo kimoja kilicho karibu na Uwoya kimeambia
Swahiliworldplanet leo asubuhi kuwa wiki kadhaa nyuma Uwoya aliandikwa na baadhi ya mgazeti ya udaku hasa ya kampuni moja kuwa ameiba simu lakini habari zile zilionekana kuwa na ajenda flani ya kumshusha star huyo kwa kuwa ziliingizwa habari na mambo mengine ambayo hayakushabihiana na tukio la wizi wa simu ambalo Uwoya wala hakusika nalo kwa kuiba simu hiyo. Na baada ya habari hiyo Uwoya akatangaza kuachana na uigizaji wa filamu ili kuyaziba mdomo baadhi ya magazeti ambayo yalikuwa yanamuandika vibaya kuwa hauzi filamu wala ma-producer hawamtaki tena kitu ambacho si kweli kwa mujibu wa chanzo hicho bali Uwoya anacheza filamu kama kawaida na ma-producer bado wanamhitaji kama zamani na hata wao walishangazwa na habari zilizoandikwa magazetini.
"Uwoya alisikitishwa sana na hali ile na hata baadhi ya watu wake wa karibu na producers walionekana kushangazwa na kilichoandikwa na media, truth ni kuwa Irene yupo kwenye filamu na anashuti kila siku lakini aliamua kutangaza vile ili baadhi ya waandishi waliokuwa na ajenda zao za kumshusha alipo wakose cha kuandika, hebu niambie wewe mwenyewe Uwoya ni mtu wa kulipwa laki moja kweli kwasasa!" Kilisema chanzo hicho
Chanzo hicho kiliendelea kwa kusema kuwa kwasasa Uwoya anashuti filamu mpya za watu kama tano na nyingine huwa anakataa kutokana na kukosa muda " Uwoya yuko busy na issue zake kibao wala hakuwa na time ya kujibizana na wale makanjanja, kuna movies za watu kama tano anashuti now, si mliona wenyewe walitaka kumharibia hata Ommy Dimpoz sema yeye aliujua mchezo haraka na kuomba radhi kwa mashabiki kumbe wala hakumaanisha kilichoandikwa magazetini, wenye upeo ndiyo wanajua pumba na mchele"
Irene Uwoya
Follow us on twitter Swahili World Planet and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP
for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities,
features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and
Nollywood news
No comments:
Post a Comment