Bashizi anasema kuwa wanatumia lugha ya kiswahili katika filamu licha ya kuwa ulaya ili kuzidi kuikuza lugha hii ambayo inawaunganisha watu wengi katika nchi mbalimbali hasa za kiafrika. Ukiachilia mbali Twin Sisters Bashiz ambaye ni muongozaji wa filamu pia ameshatengeneza filamu nyingine kama vile Jabuka, The Pain Of Love, Tears Of Money na Remember God ambayo imetengenezwa kwa lugha ya kiingereza. Angalia picha za uchukuaji wa filamu hiyo hapo chini.............
Pages
▼
Friday, September 20, 2013
TWIN SISTERS, FILAMU MPYA YA KISWAHILI KUTOKA NORWAY, YAWAKUTANISHA BASHIZI, SELEMBE TOKO, MAGGIE NA ISABELLE.
Twin Sisters ni filamu mpya ya kiswahili ambayo
imetengenezwa nchini Norway na Patrick Bashizi ambaye ni mmiliki wa
kampuni ya JDP Production. Bashizi anaishi nchini Norway lakini akiwa na
asili ya Congo. Filamu hii imechezwa na Bashizi, Selembe Toko
anayeishi Denmark na Maggie Seluwa ambaye ni muimbaji/muigizaji na isabelle Petersen .
Inatarajiwa kutoka hivi karibuni katika DVD na kuna uwezekano mkubwa
ikasambazwa Tanzania pia kama si nchi zote za Afrika mashariki na kati .
Bashizi anasema kuwa wanatumia lugha ya kiswahili katika filamu licha ya kuwa ulaya ili kuzidi kuikuza lugha hii ambayo inawaunganisha watu wengi katika nchi mbalimbali hasa za kiafrika. Ukiachilia mbali Twin Sisters Bashiz ambaye ni muongozaji wa filamu pia ameshatengeneza filamu nyingine kama vile Jabuka, The Pain Of Love, Tears Of Money na Remember God ambayo imetengenezwa kwa lugha ya kiingereza. Angalia picha za uchukuaji wa filamu hiyo hapo chini.............
Bashizi anasema kuwa wanatumia lugha ya kiswahili katika filamu licha ya kuwa ulaya ili kuzidi kuikuza lugha hii ambayo inawaunganisha watu wengi katika nchi mbalimbali hasa za kiafrika. Ukiachilia mbali Twin Sisters Bashiz ambaye ni muongozaji wa filamu pia ameshatengeneza filamu nyingine kama vile Jabuka, The Pain Of Love, Tears Of Money na Remember God ambayo imetengenezwa kwa lugha ya kiingereza. Angalia picha za uchukuaji wa filamu hiyo hapo chini.............
No comments:
Post a Comment