Saturday, September 21, 2013

GEOFREY KUSILA KUJA NA FILAMU AKIWA NA MUIGIZAJI WA NIGERIA, AFUNGUA PUB KINONDONI.

Muigizaji wa filamu nchini Geofrey Kusila anatarajiwa kuonekana katika filamu mpya akiwa na muigizaji wa Nigeria Tuvi James. Filamu hiyo inaandaliwa na Kusila kwa ushirikiano na kampuni ya Leo Media ambayo pia anafanyia kazi kama production manager. Kusila alikuwa S.Afrika hivi karibuni ambako alikutana na Tuvi na kufanya filamu hiyo.

Kwa upande mwingine muigizaji huyo ambaye ni mpenzi wa muigizaji Nuru Nassor(Nora) amefungua pub yake maeneo ya Kinondoni Biafra kona ya Hombus kama unaenda Mwananyamala karibu na jengo la SSTL Pub hiyo Inaitwa Ndoa Goli La Tatu ambapo kuna filamu wameigiza pia ikiwa na jina hilo, hivyo kwa wale watu wa kujirusha hiyo si sehemu ya kukosa.

Geofrey Kusila akiwa na Tuvi James aliyevaa kofia walipokuwa S.Afrika hivi karibuni
Baadhi ya picha kutoka kwenye pub hiyo.
 
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

No comments:

Post a Comment