Saturday, September 21, 2013

CLOUD UKWELI NI KUWA MAINDA HANA TATIZO LOLOTE ILA WEWE NA WENGINE NDIYO MNA TATIZO.

Cloud
Juzi muigizaji Issa Musa(Cloud) alikaririwa na gazeti moja pendwa akisema kuwa muigizaji mwenzake Mainda anapotea katika Sanaa licha ya kuwa na kipaji kwakuwa tu umbo lake ni dogo hivyo maproducer wengi hawampi nafasi muhimu katika filamu kama vile kucheza kama mke wa mtu ikiwemo kucheza nae yeye hawawezi kuendana kwa kuwa maumbo yao ni tofauti yaani Cloud ana mwili mkubwa huku Mainda akiwa na mwili mdogo. "Stori nyingi zinamkataa Mainda, mfano mimi siwezi kuigiza naye kama mke na mume kwani umbile lake na langu haliendani hivyo natoa wito kwa wasanii kumsaidia Mainda sababu ana uwezo mkubwa wa kuigiza" alisema Cloud

Alichokisema Cloud kina ukweli lakini kwa asilimia ndogo sana kiasi kwamba haiwezi kumuathiri Mainda hata kidogo ambaye kila mtu anajua kipaji alichonacho katika filamu. Tatizo ni kuwa hakuna professionalism katika filamu zetu na waigizaji wengi hawana malengo. Kwanini? mara nyingi waigizaji wakuu katika filamu wanapaswa kuwa na miili ya kawaida kwa kufanya mazoezi mara kwa mara ili iwe rahisi kwao kucheza characters mbalimbali na tofauti. Pia ili iwe rahisi kwa wao kucheza na waigizaji wenzao wengi wakiwemo wa jinsia tofauti kama wapenzi au wake/waume zao. Mfumo huu ni wakitaalaam sana ambao unatumiwa sana Hollywood na Bollywood kwa waigizaji hasa wakuu kufanya mazoezi, gym na diet kama sehemu ya maisha yao kwa kuwa tasnia ya filamu huchukuliwa kama taaluma nyinginezo mfano udaktari, uwanajeshi. Mazoezi pia humfanya mtu awe na afya bora na kutozeeka mapema na hili tunalishuhudia sana kwa waigizaji wa nje wana zaidi ya miaka 40 lakini wanacheza kama wanafunzi wa sekondari na kukaa vizuri tofauti na hapa kwetu muigizaji ana miaka 25 lakini kama ana miaka 40 na watoto watano.

Mazoezi ndiyo husaidia muigizaji kubadilika umbo na muonekano kwa ujumla kutokana na mahitaji ya character husika na hii tumeshudia sana waigizaji wengi wa Hollywood na Bollywood wakibadilika miili na muonekano kutoka filamu moja hadi nyingine. Ukiangalia kwa undani ni kuwa Cloud ambaye kwasasa ni mnene tena kwa kujiachia bila sababu ndiye ana tatizo ambalo sio rahisi kwa yeye kufanya filamu kimataifa au nje ya nchi kwani kuna characters nyingi hawezi kuzicheza sababu ya kuwa mnene na mzito. Cloud akipungua na kuwa na mwili wa kawaida ataweza kucheza nafasi nyingi zikiwemo za kuwa mume wa waigizaji wengi wa kike akiwemo Mainda kwa kuwa atakuwa na mwili wa kawaida tu. Mfano Ray kwa sasa amepungua ni rahisi kucheza kama mume wa Mainda tofauti na mwanzoni ambapo mwili wake haukuruhusu. Faida nyingine ya waigizaji kupungua uzito ni kuvaa mavazi mengi na kuwapendeza hata wakiwa katika events mbalimbali tofauti na ilivyo sasa wengi huonekana kituko hata katika red carpet.

Mainda kutokana na umbo lake la kawaida ni rahisi kucheza nafasi mbalimbali na kuwika hata nje tofauti na anavyobaniwa sasa kwa watu kujiona wanajua sana kumbe wao ndiyo wapo gizani. Mainda ni rahisi kucheza kama mwanafunzi wa shule ya msingi, sekondari, chuo, mke wa mtu, kucheza kama mwanamichezo, kucheza actions na characters nyinginezo. Je Cloud, JB. Rado, Wema Sepetu, Irene Uwoya, Shamsa Ford na wengineo kwa miili waliyo nayo wanaweza kucheza kama wanamichezo mashuhuri  mfano riadha, mpira wa miguu na michezo mingineyo inayomtaka mtu kuwa mwepesi na mwili wa kawaida? jibu ni hapana kwa kuwa hawana miili au muonekano wa kiuwanamichezo lakini Mainda ni rahisi kufanya maajabu kuliko hao kwa kuwa mwili wake ni rahisi kumcheza characters nyingi na akakaa vizuri.

Kingine ambacho ni cha muhimu sana pia ni kutowatumia wataalaam wa mavazi na mapambo katika filamu ambao jukumu lao ni kumvalisha na kumpamba muigizaji ili aendane na uhusika. Hawa huweza kumfanya muigizaji aonekane mdogo au mkubwa kupitia mavazi na mapambo. Na sio kama ilivyo sasa katika filamu zetu muigizaji anajipamba mwenyewe au make up designer kazi yake ni kumpaka poda, wanja na lipstic pekee muigizaji. Mfano Mariam Ndaba blogger maarufu wa Missiepopular ni mtaalaam mzuri sana wa mavazi katika filamu akiwa amesomea Chuo kikuu cha Dar es salaamm lakini hakuna mtengenezaji wa filamu Tanzania anayemtumia sababu ya kuendekeza kujuana na kutoheshimu professionalism kwa kisingizio kuwa budget ni ndogo lakini je ulimtafuta na kuzungumza nae vizuri ili kufanya kazi bora?. Missiepopular ndiye amefanya kazi nzuri ya mavazi katika filamu ya Going Bongo kwa waigizaji zaidi ya 50 ndani ya filamu hiyo. Lakini filamu ya waigizaji 10 tu anashindwa kutumiwa na waandaaji wa filamu nchini ili kufanya kazi bora.

Kwa ufupi ni kuwa waigizaji wetu wanatakiwa wawe na miili ya kawaida kwa kufanya mazoezi na diet ili kuwa na mvuto kama mastaa mbele za watu, mavazi kuwapendeza na wao kuwa rahisi kucheza uhusika tofauti. Kuna baadhi ya filamu Cloud mwenyewe amecheza lakini mwili wake haukuendana na characters hizo sawa na Ray, Jb na wengineo kuna filamu wamecheza lakini hawakuendana na characters hizo sema kwakuwa wao ndiyo watengenezaji basi walijipa nafasi hizo muhimu ambazo zilitakiwa kuchezwa na wengine. Kama kuwa na umbo dogo ni tatizo kwa muigizaji basi Jackie Apiah na Majid Michael wa Ghana wasingefanikiwa. Shahrukh Khan, Aamir Khan, Shahid Kapoor wasingefanikiwa kwa kuwa wote wana miili midogo. Lakini wenzetu huangalia kipaji na mazoezi ni sehemu muhimu kwa waigizaji. Shahrukh Khan amecheza na waigizaji wengi wa kike warefu kama mume wao na kukaa vizuri sawa na Jackie Apiah ambaye licha ya kuwa mfupi amecheza na waigizaji wa kiume wenye miili mikubwa kama mke na kufanya vizuri kuliko hata kina Omotola Jalade na Mercy Johnson wenye miili mikubwa.

Katika filamu ya Nguvu Ya Imani iliyotoka hivi karibuni Simon Mwapagata(Rado) aliigiza kama mume wa Kemmy lakini licha ya wote kuwa na miili mikubwa Rado alichemka katika character yake huku Kemmy akionyesha maajabu ya kipaji chacke. Sudi Ally au Steve Nyerere kama mmoja wao angecheza kama mume wa Kemmy angeweza kukaa vizuri licha ya kuwa na miili midogo kama tu angepata director mzuri, ,mtaalaam wa mavazi na mapambo mwenye ujuzi. Ushauri ni kuwa tubadilike kwa kuongeza elimu yetu kuhusu tasnia ya filamu, Tuwathamini na kuwatumia wataalaam waliopo sasa na kutoa kipaumbele kwenye vipaji na sio kuangalia muonekano mzuri au uzuri na ukubwa wa umbo la mtu. Waigizaji wafanye mazoezi ili kuwa na miili ya kawaida kuwarahisishia kucheza uhusika tofauti, kuwa wepesi na kuwa na mvuto mbele za watu

                                       Mainda
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

No comments:

Post a Comment