Monday, September 9, 2013

ACTRESS AISHA BUI ADAIWA KUFUNGWA NCHINI BRAZIL BAADA YA KUKAMATWA NA UNGA, MCHUMBA WA PENDO MOSHI ADAKWA CHINA NA MADAWA YA KULEVYA.

Mchumba wa mwigizaji wa filamu Swahiliwood Pendo Mushi ‘Pendo wa Maisha Plus’ aliyejulikana kwa jina moja la Tasha amedakwa na unga nchini China.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, Tasha alikamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Beijing nchini humo akiwa na unga aina ya heroin (kiasi na thamani hakikutajwa).
Ili kupata uhakika wa madai hayo Ijumaa Wikienda lilimtafuta Pendo kwa njia ya simu ya mkononi na kumuuliza kuhusu madai hayo ambapo alikiri.
“Yeah, ishu ni kweli. Mimi nilizipata hizo taarifa kutoka kule nikawaambia ndugu zake. Kwa mujibu wa mtu wake aliyekuwa naye kule (China) jamaa (Tasha) ameshapandishwa kortini,” alisema Pendo huku akisema uchumba wake na Tasha ulishakufa.
Pendo

AISHA BUI ETI KAFUNGWA BRAZIL!
Wiki mbili sasa, mapaparazi wa Global Publishers wamekuwa wakifuatilia kwa undani kuhusu kusambaa kwa madai kwamba, staa wa filamu Swahiliwood, Aisha Bui eti kafungwa miaka 5 jela katika gereza moja nchini Brazil baada ya kukamatwa na madawa ya kulevya kwenye kibegi.
Kwa mujibu wa madai ya habari hizo, eti Aisha alidakwa kwenye uwanja wa ndege wa jijini Brasilia akirejea Tanzania kupitia Dubai.
Septemba 2 na 5, mwaka huu, waandishi walifika nyumbani kwa baba wa Aisha, Kigamboni, Dar kutaka kujua ukweli.
Septemba 2, mtu aliyekutwa nyumbani hapo alisema Aisha yupo Brazil lakini hakuna mawasiliano naye na alikwenda siku chache kabla ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, Julai mwaka huu.
Septemba 5, hakukutwa mtu ila majirani walielekeza eneo analopatikana mzee huyo ambapo ni ufukweni. Hata hivyo, sehemu hiyo hakupatikana na waandiishi waliacha namba zao za simu.

Jioni, mzee Bui alizipata namba zilizoachwa, saa 9:00 usiku wa kuamkia Septemba 6 alimpigia simu mwandishi wetu na kumvurumishia matusi huku akisema akome kumfuatafuata akidai yeye hana mawasiliano na binti yake tangu mwaka 2007.
Mzee huyo alikwenda mbele zaidi kwa kutuma ujumbe mfupi wa simu (SMS) kwenye simu ya paparazi akitumia lugha ya Kiarabu ambapo kwa mujibu wa wataalam wa lugha hiyo ni dua ya kumwombea mabaya mwandishi huyo.

Ili kwenda mbele zaidi, mapaparazi walikwenda ofisini kwa Kamanda wa Kikosi Maalum cha Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa ili kutaka kujua kama amesikia lolote kuhusu Aisha Bui.
Alisema: Eee, kuna habari kama hiyo lakini si rasmi kwangu, bado nafuatilia Brazil ikiwa tayari nitawajulisha tu.
Ijumaa Wikienda lilimtafuta Aisha kwenye mitandao, hasa Facebook, Instagram na Twitter bila mafanikio. limemwachia ujumbe kwa kuamini kwamba akirudi hewani ataukuta na kujibu lakini wapi!
                                                        Aisha Bui

  Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood new

No comments:

Post a Comment