Pages

Thursday, August 8, 2013

WEMA SEPETU HATUMII MKOROGO KABISA: MARTIN KADINDA

Kadinda na Wema
Mbunifu wa mavazi nchini Martin Kadinda ambaye pia ni meneja wa Wema Sepetu ameamua kufunguka kuwa Miss Tanzania 2006 na sasa muigizaji wa filamu Wema Sepetu hajawahi kutumia mkorogo na dawa za kichina na wala hajazeeka kama watu wanavyodai. Kadinda alisema yeye anamuona kigoli ingawa ngozi yake inabadilika kulingana na umri unavyokwenda. Mbunifu huyo alisema Wema wa miaka sita iliyopita hawezi kuwa wa sasa kwani umri unakatika, hivyo haamini kuwa anatumia dawa hizo ambazo wanawake wengine wanazitumia kwa lengo la kuongeza weupe. Alisema kwamba kwa upande wake anamtazama msanii huyo kama mtoto anayekuwa hivyo kutumia vipodozi ni style yake ingawa hajawahi kumuona au kumkuta akizungumzia dawa za kichina za kuongeza weupe.

"Wema mbona bado kigoli unajua naweza kusema mimi si fundi wa vipodozi lakini mtazamo wangu naamini kwamba mwanadamu hawezi kuwa na ngozi ile ile kwa muda wa miaka sita lazima atabadilika, ndiyo ilivyo kwa Wema" alisema Martin. Hata hivyo aliongeza kuwa endapo Wema angekuwa anatumia mkorogo angekuwa ameacha kitambo kutokana na madhara yanayoonekana kwa wanawake wengine ambao wanatumia kemikali hizo. "kwa ninavyomjua "best" yangu Wema sidhani kama anaweza kutumia hizo kitu kwa sababu madhara yake nayajua hivyo si mtu wa ujinga huo na watu wamekuwa wakisema sana ila naweka wazi kwamba hatumii kabisa" alisema Kadinda. Angalia picha za Wema hapo chini alivyokuwa mwaka 2006 na alivyo sasa.

credit: Sani

                                                                 Mwaka 2006
                                                   kuanzia 2011
                                               mwaka 2013

  Like our facebook page Swahili World Planet for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

No comments:

Post a Comment