Yobnesh Yusuph(Batuli) ambaye ni actress maarufu Swahiliwood
amemuomba Rais Jakaya Kikwete alivunje Baraza la Sanaa la Taifa(BASATA)
na kuliunda upya. Leo kupitia akaunti yake ya twitter muigizaji huyo
aliyejaaliwa mvuto na kupendwa na mashabiki wengi wa filamu ali-tweet
moja kwa moja akimtaja JK kwa kuandika "ujumbe wa sikukuu ya Eid kwako
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, vunja baraza la
BASATA uliunde upya".
Ingawa Batuli hakutaja moja kwa
moja kwanini baraza hilo linalosimamia sanaa ikiwemo tasnia ya filamu
nchini livunjwe lakini kwa muda mrefu wasanii wakiwemo wa filamu na
muziki wamekuwa wakililalamikia baraza hilo kuwa linafanya mambo
kienyeji na baadhi ya wasanii kudai kukumbana na urasimu wanapotaka
kufanya kazi zao za sanaa. Wengine wanadai hata hatua iliyopigwa sasa
katika sanaa nchini ni juhudi za wasanii wenyewe pasipo sapoti ya
kutosha kutoka BASATA. Baadhi ya wasanii wa filamu wamekuwa pia wakitaka
TAFF ndiyo ipewe mamlaka kamili ya kusimamia shughuli zote za tasnia ya
filamu nchini kutokana na BASATA kuwepo muda mrefu lakini Sanaa ya
Tanzania bado haijapewa hadhi ya sekta rasmi na kuwa na sera ya
kueleweka katika kumkomboa msanii na kuzidi kupiga hatua.
Hivi
karibuni pia mwanamuziki Diamond Platinumz alikaririwa akisema BASATA
ndiyo wa kulaumiwa kwa kutokuwa na tuzo nyingine za muziki mpaka sasa
kwakuwa chombo hicho kimekuwa kikiweka kauzibe kwa watu wanaotaka
kuazisha tuzo mbalimbali za sanaa ikiwemo hata katika tasnia ya filamu.
Kama wewe ni shabiki wa Batuli basi m-follow hapa BATULI-ACTRESS katika mtandao wa twitter ili kupata updates zake
Like our facebook page Swahili World Planet
for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities,
features, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news
Good girl today your talking Mrs Slim Jk vunja Basata
ReplyDeleteSAMAHANI MWENYE BLOG BATULI ANAPHOTOS NYINGI HII UNAIPENDA SANA USITUFANYIE HILA WELL POLENI WASANII BASARA YAONYESHA NI KIKWAZO KIKUBWA SANA KWENU
ReplyDeleteYou are a strong woman Batuli
ReplyDeleteKeep it up girl umetupa jiwe mahala pake hamnufaiki na Basata mnaibiwa na haki miliki zenu zinamilikiwa na muhindi Mr President aache kucheka cheka sasa panga tu
ReplyDeleteBE BLESSED GIRL I LOVE THE WORDS HON JAKAYA KIKWETE SIKILIZA KILIO CHA NYOTA WETU AT THE END OF THE DAY MNAWATUMIA KWENYE KAMPENI WAFUTENI MACHOZI YAO. HUYU KAAMUA KUKUANDIKIA UJUMBECWA WAZI ON TWITTER SHE IS A STRONG WOMAN ANA MAUMIVU YA KUTOSHA UAMUZI WA KUTWEER LIVE NI MGUMU SANA NI SAWA NA MFUNGWA ALIYETUMA BARUA YA WAZI KWAKO KUPITIA GAZETI WAONEE HURUMA WASANII WETU WANAKUFA WAKIWA HAWANA KITU. MY NAME IS JAMES E. MSUYA
ReplyDeletetatizo TZ tuna msanii sio wasanii... mnakera bwana y msifight as a team¿ midiocre
ReplyDeletePOLENI WASANII WETU KWANI BASATA NI NINI? NIELEWESHENI WACHANGIAJI WENZANGU
ReplyDeleteGreat Batuli
ReplyDelete