Pages

Wednesday, August 14, 2013

WATAYARISHAJI WA FILAMU WAANZA KUMTAKA FEZA KESSY KATIKA FILAMU ZAO.

Habari ni kuwa baadhi ya ma-producer wa filamu Swahiliwood wameanza harakati za kumtaka Feza Kessy katika filamu zao. Mtoa habari hizi ambaye yupo karibu na baadhi ya watayarishaji wenye majina makubwa nchini alisema kuwa Feza ana vigezo vingi vya kucheza filamu licha ya kuwa mwanamuziki pia. Aliongeza kwa  kusema kuwa Feza anajiamini vizuri, ni mzuri na ana mvuto mbele ya kamera na tayari ana mashabiki wengi ndani na nje ya nchi hivyo ni rahisi kufanya vizuri katika game. "watayarishaji wa filamu Bongo wameanza kumtaka Feza katika filamu zao mpya, siunajua Feza ni kifaa, ni mzuri wa asili na mvuto anao wa ukweli, anajiamini vizuri na mashabiki wengi ndani na nje ya nchi anao so ni simple sana kwake kufanya vizuri kama akiamua. Yule.... na....(akiwataja majina baadhi ya waandaaji wa filamu) tayari wanataka kumtumia Feza katika filamu zao mpya." chanzo hicho kilichokataa kutajwa jina lake kiliiambia Swahiliworldplanet jana.

Hata hivyo waandaaji hao wa filamu ambao pia wana majina makubwa kama waigizaji walipotafutwa ili kupata yaliyo upande wao mmoja hakupatikana na mwingine alisema asingependa kuliweka wazi suala hilo kwasasa na atalizungumzia akishakaa pamoja na Feza kikazi na kila kitu kuwa sawa.

Feza Kessy alikuwa mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Big Brother Africa(The Chase) na alitolewa jumapili iliyopita. Na kama Feza ataingia katika tasnia ya filamu basi atakuwa amefuata nyayo za watangulizi wake kama Mwisho Mwampamba na Richard Bezuidenhout ambao tayari wamecheza filamu kadhaa na nyingine kutamba sokoni. Feza anatarajiwa kurudi Tanzania leo na tangu juzi alikuwa anahojiwa na media mbalimbali nchini South Africa na hata kukutana ana kwa ana na mashabiki wake.

                                                               Feza
 Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies swp for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

No comments:

Post a Comment