Pages

Wednesday, August 14, 2013

ACTRESS EFRANCYAH MANGII AJITOSA KATIKA MUZIKI WA BONGOFLEVA.

Efrancyah Mangii ambaye ni muigizaji wa filamu ameamua pia kuingia katika muziki wa Bongofleva akitarajia kuimba mahadhi ya Afro pop. Akizungumza na Swahiliworldplanet Efrancyah alisema kuwa kwasasa yupo katika mazoezi makali na wiki ijayo anatarajia kuingia studio. Aliongeza kwa kusema kuwa atamshirikisha mwanamuziki mwingine lakini hakuwa tayari kuweka jina la msanii atakayemshirikisha kwa wakati huu.

Kuingia kwa Efrancyah kwenye tasnia ya muziki kunazidi kuongeza idadi ya wasanii wa filamu waliojitosa katika muziki pia kama vile Shilole, Aunt Ezekiel, Snura Mushi, Kingwendu, Bambo, Mzee Magari, na pia Wema Sepetu yupo mbioni kuachia wimbo wake.

                                                             Efrancyah
 Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies swp for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

1 comment:

  1. HAPO SIJAONA LIPS NIMEONA PUA.
    KONDA KIDOGO MY DEAR UISHI NA AFYA

    ReplyDelete