Pages

Friday, August 16, 2013

FEZA KESSY AZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI LEO (PHOTOS)


FEZA
Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi akizungumza na waandishi wa habari ambapo amewashukuru wateja wote DStv na Watanzania walioshiriki katika kumpigia kura mshiriki aliyeiwakilisha Tanzania kwenye shindano la Big Brother The Chase Season 8 Feza Kessy ambaye alibakiza siku chache tu kuweza kufuzu 14 mpaka kumalizika kwa shindano hilo. Barbara Kambogi ameowaomba wateja wa DStv waendelea na Watanzania kwa ujumla isiwe mwisho wa kutazama mchezo huo kwa sababu washiriki wa Tanzania wametoka. Katikati ni Mshiriki wa Tanzania kwenye shindano la Big Brother The Chase Feza Kessy na Kulia ni Mwakilishi wa kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania ambao ndio wadhamini  wakuu wa shindano hilo.

DSC_1061
Mshiriki wa Tanzania kwenye shindano la Big Brother The Chase Feza Kessy akizungumza na vyombo vya habari ambapo amewashukuru Watanzania wote walioshiriki kumpigia kura alipokuwa kwenye jumba hilo pamoja na familia yake  kwa kumpa ushirkiano na kusisitiza kuwa kushiriki shindano hilo halijambadilisha bali amezidi kujifunza tamaduni mbalimbali kutoka kwa washiriki wenzake na ataendelea kuwa Feza Kessy kama mwanzo.
DSC_1053
Mwakilishi wa Airtel Tanzania ambao ndio wadhamini wakuu wa shindano la Big Brother The Chase akitoa shukrani kwa Wateja wa Airtel na Watanzania kwa ujumla walioshiriki kumpigia kura Feza

credt:fresh120media
 Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies swp for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

No comments:

Post a Comment