Wednesday, July 17, 2013

WALTER DE NGONDE NDANI YA FILAMU YA HARD PRICE, AKIWA NA RAY, WOLPER NA SABBY ANGEL.

Muigizaji chipukizi wa Swahili movies Walter de Ngonde ambaye tayari ameshaigiza filamu kadhaa na mastaa wakubwa kama vile Blandina Chagula(Johari), Irene Uwoya, Cloud anatarajiwa kuonekana tena katika filamu mpya ya Hard Price ambayo pia yupo Vicent Kigosi(Ray), Jackline Wolper na Sabby Angel ambaye pia ni mwigizaji Chipukizi.
Walter ambaye tayari ni model aliyetokea katika matangazo mengi ya Tv, billboards pia alikuwa mshiriki wa Dume Challenge amesema kuwa lengo lake ni kutamba kwenye tasnia ya filamu za kiswahili licha ya kwamba kwasasa kazi aliyosomea inambana kidogo lakini lengo lake ni kujitanua kwenye filamu ili iwe ajira yake rasmi.

 Muigizaji huyo amesema kuwa lengo lake sio kutamba katika filamu za Kiswahili pekee bali anataka kujitanua zaidi kimataifa ili kufikia malengo na ndoto zake hivyo mashabiki wake watarajie makubwa kutoka kwake "ndio mwanzo wakuja katika filamu na wategemee mapinduzi katika industry ya movies hapa tanzania na kimataifa kiujumla coz malengo yangu sio kuonekana kwenye movies za bongo tu nataka kujitanua zaidi kimataifa ila Mungu ndio kila kitu nikizingatia na juhudi zangu binafsi katika kukamilisha malengo yangu japo mwanzo ni mgumu sana" alisema Walter



No comments:

Post a Comment