Wednesday, July 17, 2013

SABBY ANGEL, KIFAA KIPYA SWAHILIWOOD, KUTIKISA NA RAY, WOLPER NA DR.CHENI KATIKA HARD PRICE NA NIMEKUBALI KUOLEWA.

Wakati baadhi ya waigizaji wakongwe wakionekana kubweteka kwa kuridhika na walipofikia sasa vipaji vipya vimekuwa vikiibuka kila siku na kuleta changamoto kwa wakongwe hao. Moja ya vipaji hivyo vipya ni Sabby Angel ambaye amepata bahati ya kuanza safari yake katika film industry kwa kuigiza na mastaa wakubwa huku akipata nafasi ya uhusika mkuu(heroine) katika filamu ya "Hard Price" akiwa na Vicent Kigosi(Ray) na Jackline Wolper. Ukiachilia mbali Hard Price actress huyo pia ameigiza na Muhsin Awadhi(Dr.Cheni) ambaye ni star mkubwa Swahiliwood katika filamu ya "Nimekubali Kuolewa" ambayo pia inatarajiwa kuingia sokoni muda si mrefu. Filamu hizi zote mbili zinatarajiwa kumtambulisha vizuri katika game muigizaji huyo aliyejaaliwa mvuto . Angalia picha zake hapo chini......................


No comments:

Post a Comment