Monday, July 29, 2013
SINA MPANGO WOWOTE WA KUOLEWA: MONALISA
Yvonne Cherryl(Monalisa) ambaye ni actress maarufu wa filamu za Swahiliwood amesema kuwa hana mpango wowote wa kuolewa kwasasa kama alivyotania wakati wa send off ya mama yake Suzana Lewis(Natasha) ambaye aliolewa hivi karibuni. Katika vikao vya maandalizi ya send off ya mama yake muigizaji huyo wa siku nyingi na asiyechuja alitania kuwa na yeye anaolewa December mwaka huu. "Sina mpango wa kuolewa kabisa, kwanza sina mchumba nitaolewaje? siku ile nilikuwa natania tu kwasasa sipo tayari kwa tendo hilo" alisema Monalisa akiongea na Globalpublishers. Muigizaji huyo huko nyuma aliwahi kuolewa mara mbili na kubahatika kupata watoto.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment