Monday, July 15, 2013

NACHUKIA KUKAA KATIKA MAKUNDI AMBAYO HUWEZA KUNIHARIBIA SWAUMU YANGU: SHAMSA FORD

Muigizaji Shamsa Ford amesema kuwa katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani huwa anahakikisha anafunga na kufanya ibada mara kwa mara. Akizungumza na Swahiliworldplanet Ford aliendelea kwa kusema kuwa katika mwezi huu anachukia kukaa katika makundi ambayo ni rahisi kumharibia swaumu yake. "ninachofanya ni kufunga na kufanya ibada, pia nachukia mwezi huu kukaa katika makundi ambayo yataniharibia swaumu yangu" alisema actress huyo ambaye tayari ameigiza filamu Swahiliwood. 


No comments:

Post a Comment