Lulu na mama Kanumba
Monday, July 29, 2013
LULU NA MAMA KANUMBA WAJIMWAGA KUCHEZA WIMBO WA GOSPEL.
Uhusiano kati ya mama Kanumba na muigizaji Elizabeth Michael(Lulu) unazidi kukua kila siku utadhani ni mtu na mama yake mzazi. Lulu hivi karibuni kupitia kipindi cha Take one alisema mungu akijaalia siku za karibuni atakuja kuigiza filamu pamoja na mama Kanumba na hawezi jua anaweza kuja kuimba nyimbo za injili pia. Ukiachilia mbali hayo habari mpya ni kuwa Lulu na mama Kanumba wamenaswa wakicheza wimbo wa injili pamoja na video ikiwaonyesha wakicheza imeanza kusambaa mitandaoni hivyo tukiipata tutakuwekea hapa ujionee. Hii inaonyesha kuwa hakuna tatizo kati yao na wote wamesahau na kumwachia Mungu yaliyopita. Hii picha pia ni ya hivi karibuni ikiwaonyesha wawili hao wakiwa na furaha tele.
Lulu na mama Kanumba
Lulu na mama Kanumba
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment