Saturday, July 6, 2013

KAMPUNI ZA NJE ZAVUTIWA KUFANYA KAZI NA MUIGIZAJI LUCY KOMBA.

Lucy Komba ni actress maarufu wa filamu za Swahiliwood ndani na nje ya nchi huku akizidi kujitanua kila siku kwa kufanya kazi na wasanii wa mataifa mbalimbali kama vile Denmark. Kwasasa muigizaji huyo aliyewaibua waigizaji maarufu kama vile Irene Uwoya na Jackline Wolper yupo nchini Denmark kwa mapumziko ya miezi mitatu. Pia tayari ameshafanya kazi na waigizaji wa nchi kadhaa za kiafrika na anashirikiana kwa ukaribu na VAD Productions ya nchini Denmark. Swahiliworldplanet ilipata nafasi ya kuwasiliana na muigizaji huyo akiwa nchini humo na kumuuliza machache kuhusiana na safari yake hiyo kama ifuatavyo.......

SWP: Mashabiki wako wangependa kujua huko Denmark unafanya film nyingne au ?

LUCY:  Nimekuja kupumzika tu nitarudi baada ya miezi mitatu lakini kuna kampuni tatu zinataka kufanya kazi na mimi kipindi hiki lakini nitaangalia kwani lengo langu nikupumzisha kichwa changu kwanza.

SWP:  Wow...... hilo ni jambo zuri sana mungu kuzidi kukufungulia milango ya mafanikio. So kampuni hizo zote ni za Denmark au?

LUCY:  Ni watanzania ambao wanaishi/raia wa huku, za wadenish wenyewe ni ngumu kwa vile wao wanaongea kidenish kwenye filamu zao. Hawatumii kiingereza na pia hawakijui vizuri, viingereza vyao ni vya kubabaisha kama vyetu.

SWP: So mikakati yako pia ni kuingia Hollywood siku za usoni ?

LUCY:  Ndiyo Mungu akipenda natamani sana niingie Hollywood.

SWP:  Inshallah mungu atasaidia na vipi kuhusu filamu ya "From Tanzania To Denmark" imepokelewa vizuri na mashabiki wa huko ndiyo maana hizo kampuni zinataka kufanya kazi na wewe na kuzidi kukubalika huko?

LUCY:  Sana na hasa ilipofanyika interview watu wengi walihudhuria na wameipenda sana na wameshaanza kuulizia nakala(copy) kwa wingi. Kwa bahati mbaya uzinduzi sikuweza kuwahi kutokana na Visa yangu kuchelewa na watu walisikitika kunikosa kwani walikuja kwa wingi wakitegemea watamuona Lucy Komba,
na baadhi walikuwa wanarudi njiani baada ya kuwasiliana na wenzao na kuambiwa Lucy Komba hayupo ukumbini. Watu wanaulizia kopi ya Tanzania to Denmark kwa wingi lakini sasa hivi nimekuja nimeshapigiwa simu watu wengi wanataka kuniona na ndiyo maana hata kampuni nyingine zimepata moyo wa kufanya kazi na mimi.

SWP: Hii inaonyesha ni jinsi gani unakubalika hata nje ya nchi. So kuwa huko pia ni mikakati ya kuzidi kutafuta wasambazaji wa kazi zako ili zifike mataifa mengi zaidi ukifikiria bado usambazaji wa filamu huku Tanzania sio wa kuridhisha?
LUCY:  Ni kweli usambazaji Tanzania unazidi kukatisha tamaa, naendelea kufuatilia nione litakalowezekana.

We wish the Swahiliwood diva all the best
Lucy Komba

No comments:

Post a Comment