Saturday, July 6, 2013

EXCLUSIVE: JOKATE KUJIKITA RASMI KWENYE MUZIKI.

Baadhi ya Mashabiki wa Jokate Mwegelo wamekuwa wakiulizia kuhusu Jokate kutokuonekana kwenye filamu mpya licha ya huko nyuma kucheza filamu kadhaa zilizoandikwa sana kwenye media na nyingine kutwaa baadhi ya tuzo. Filamu alizoigiza modo huyu, mbunifu na mtangazaji maarufu ni kama vile From China With Love, Fake Pastors na Chumo. Swahiliworldpanet iliamua kumuuliza mrembo huyo maarufu ndani na nje ya nchi na alisema kuwa kwasasa kuna nyimbo zake anazifanyia kazi ambazo ameimba mwenyewe na nyingine ameshirikisha baadhi ya wasanii "kuna nyimbo zangu nazifanyia kazi, nimeimba mwenyewe na nyingine kushirikisha" alisema Jokate ambaye hajawahi kuchuja kwenye umaarufu tangu 2006 aliposhindana katika mbio za Miss Tanzania.
 
Hii ni ishara kuwa Kidoti ambaye pia ni mtangazaji wa Channel O ameamua kujikita rasmi kwenye muziki pia kama biashara tofauti na huko nyuma alishirikishwa zaidi na hakuwa active.We would like to wish the diva all the best





No comments:

Post a Comment