Friday, July 5, 2013

KAJALA AONEKANA NA TATTOO LICHA YA KUIGIZA KAMA MSICHANA WA KIJIJINI ! ANAFUATA MKUMBO WA IRENE UWOYA AU WEMA SEPETU !

Kajala Masanja ameweka picha za filamu yake mpya Instagram, filamu hiyo inaitwa Heart Attack na mastaa wengine katika filamu hiyo ni pamoja na Jengua, Bi. Mwenda, Thecla Mjata na Hemed. Katika filamu hiyo inaonekana Kajala amecheza kama msichana wa kijijini huku akipitia mateso mengi kutoka kwa Jengua. Hata hivyo kilichoanza kushangaza watu ni Kajala kuwa na tattoo mkononi licha ya kucheza kama msichana wa kijijini ambapo si rahisi kwa mtu wa mazingira ya kijijini kuonekana na urembo au pambo la tattoo. Haijajulikana kama uhusika wake umemtaka awe na hiyo tattoo au ameamua kuendeleza tu ile tabia ya "bora liende".

 Kumekuwa na ni hii tabia baadhi ya waigizaji kujichora tattoo maeneo ambayo ni rahisi kuonekana na hivyo wanapoigiza katika filamu kuathiri au kuharibu characters zao ambazo haziruhusu michoro hiyo na hivyo kuishia kuonekana kweli "wanaigiza" na siyo kufanya filamu. Waongozaji wa filamu hizo nao haieleweki kuwa wanapenda kulipua kazi au vipi. Tattoo zao ni rahisi kuzibwa na nguo kama filamu husika ina mtu wa mavazi aliye makini au editor wa filamu pia anaweza kufanya special effect ili zisionekane lakini huwa haiwi hivyo. Ukiachilia Kajala baadhi ya waigizaji wengine ambao mara nyingi tattoo zao zimekuwa zikionekana kwenye characters zisizoruhusu ni pamoja na Irene Uwoya na Wema Sepetu. Mfano Wema Sepetu katika filamu ya "It Was Not Me" amecheza kama mwanafunzi wa chuo huku tattoo zake zikionekana. Irene Uwoya katika filamu ya Sobbing Sound alikuwa pia ni mwanafunzi huku tattoo zake zikionekana wakati characters zao wote hazikuhitaji urembo huo hivyo kuishia kukosa nguvu na uhalisia wa kile walichoigiza.

Ushauri wa bure kwa waigizaji wetu ni kuwa wanapojichora hii michoro wachague maeneo ambayo sio rahisi kuleta tabu wanapoigiza filamu. Pia ikumbukwe kuwa hata nchini Marekani fasheni ya kujichora tattoo imeenea zaidi kwa wanamuziki na siyo waigizaji wa filamu ambao inawalazimu kuifuta mara kwa mara pale wanapoigiza characters zisizoitaka michoro hiyo inayodaiwa kuwa na athari mbaya kwa mhusika.
 Angalia picha za kajala akiwa na tattoo kutoka filamu ya Heart Attack.........


No comments:

Post a Comment