Pages

Thursday, July 25, 2013

IRENE UWOYA ARUDI NCHINI, MFALME MSWATI WA SWAZILAND AAHIDI KUMSAPOTI KATIKA KAZI ZAKE ZA FILAMU.

Actress maarufu Swahiliwood Irene Uwoya tayari amerudi nchini leo hii akitokea Swaziland alikokuwa kwa takribani wiki tatu sasa. Muigizaji huyo amesema kuwa mfalme Mswati wa Swaziland anawasalimia sana na pia amempa kibali cha kufanya filamu. Pia mfalme Mswati atampa Uwoya sapoti ya kutosha katika filamu hiyo. Muigizaji huyo mwenye mashabiki wengi nchi mbalimbali za Afrika mashariki na kati amesema kuwa muda ukifika wabaya wake watajuta. "Mswati anawasalimu sana! na hivi karibuni atatinga hapa na kanipa kibali cha kufanya movie na full support......i will prove you wrong.... trust me". aliandika Uwoya katika mtandao mmoja wa kijamii.

Tumejaribu kumtafuta Uwoya ili atoe ufafanuzi zaidi kuhusiana na kauli yake hiyo kuhusu Mfalme Mswati kusapoti kazi zake za filamu lakini namba yake haipatikani hewani. Lakini tukimpata tutakuletea story nzima kuhusiana na safari yake nzima. Ingawa haijajulikana wazi alichofuata Uwoya huko lakini wiki kadhaa nyuma aliwahi kusema yeye na kina Johari watakuwa na ziara katika nchi kadhaa za kiafrika kuchunguza soko la filamu za kiswahili na kujifunza kwa wenzao wa huko pia ili wazidi kuongeza soko la filamu za kiswahili nchi mbalimbali.

 Like our facebook page Swahili World Planet for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, fashions plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment