Pages

Thursday, July 25, 2013

HII NDIYO KAULI YA LUCY KOMBA KUHUSU MADAI YA IRENE UWOYA, IRENE APONDWA NA WATU.

Jana mtandao wa Globalpublishers ulitoa habari ukimnukuu Irene Uwoya akisema kuwa muigizaji mwenzake Lucy Komba ana lengo la kumzunguka na kumharibia ndoa yake sababu ikiwa ni Lucy Komba kucheza filamu pamoja(Kwanini Nisimuoe) na Hamad Ndikumana raia wa Rwanda ambaye alimuoa Irene Uwoya na mara kwa mara magazeti na mitandao kuripoti kuwa wametengena ingawa haijadhibitika rasmi mpaka sasa kama ni kweli wametengana sababu kubwa ikidaiwa ni skendo za mara kwa mara za Uwoya zinazoripotiwa magazetini. Baada ya habari hizo kuenea kwenye mitandao jana Swahiliworldplanet iliamua kuzungumza na Lucy Komba kutokea nchini Denmark alipo sasa ili kupata maoni ya upande wake baada ya habari hiyo. Kwanza Lucy alionekana kama kushangazwa na kauli ya Uwoya halafu alicheka na kusema kuwa hata yeye yupo nje ya nchi kama Uwoya ambaye yupo Swazland kwasasa hivyo hawezi zungumzia suala hilo mpaka atakaporudi nchini ndiyo atazungumzia suala hilo "Ha ha nimesoma Siwezi kuongea chochote kuhusu Hilo kwani hata mimi sipo Tanzania nikirudi ndo nitaliongelea hilo" alisema Lucy Komba ambaye ndiye aliyemuingiza Uwoya kwenye filamu akitokea kwenye umiss.

Hata hivyo historia inaonyesha kuwa Lucy Komba ameibua vipaji vingi vya filamu nchini kutoka katika kada mbalimbali kama vile muziki, mitindo na hata waigizaji wengine chipukizi wasiotokea katika fani nyingine kwa kuwapa nafasi ya kucheza katika filamu zake mbalimbali akiwemo Uwoya mwenyewe hivyo hatudhani kuwa ni tatizo kama ameona kipaji cha Ndiku na kuamua kukiendeleza. Nakuhusu madai ya Irene kuwa Lucy hakumueleza kuhusu kucheza filamu na mumewe hili linaweza kuwa jukumu la Ndiku mwenyewe kwani ni mtu mzima na kama mume. Na kama kweli amekuja nchini na kucheza filamu bila kumwambia Irene wala kumshirikisha ni lazima kutakuwa na walakini kwa wanandoa hao maana ni jambo lisilowezekana mume atoke nchi nyingine na kuja nchi anakokaa mkewe bila kuonana tena akifanya kazi kubwa ya filamu ambayo mwisho wa siku ni lazima iwe hadharani kwa mashabiki(public) akiwemo mkewe kuitazama.

Ukiachilia hayo hapo juu baadhi ya watu wakiwemo wasanii wawili waliokataa kutajwa majina yao walituma ujumbe SWP baada ya kusoma habari hiyo na kusema.....

Msanii 1: "ha ha ha haaaa, Uwoya asijifarague kwa kutafuta pa kufichia aibu yake, alishampa stress mwanaume wa watu kwa kujitia star mara kibao, alishaharibu ndoa yake tangu siku nyingi mbona !"

msanii 2: Looh.... haya makubwaaa! amesahau ya hivi karibuni tu kwa Diamondoooo......! shauri yake wenzake wanataka ndoa ye anaichezea, na kama Ndiku ni kweli anatoka na Lucy basi kaona anamfaa.

Katika mitandao mbalimbali iliyoweka habari hiyo jana baadhi ya maoni ya watu ni  hayo hapo chini.......

Dosca Kusenha: aache uhuni mbona yeye aliduu na Diamond...amuache dada etu kwanza hana kawaida ya kula vilivyoliwa

Sam Mdee: kila mla vya wenzie ajue na vyake vtaliwa

Sikitu Husein: Uwoya hana akili mi naonaa .....kama kweli anampenda ndiku na ndoa yake why anatumia jina la Irene wa Ferola ktk Instagram wakat feregola ni jina la mwanaume mwingine wa Congo, y asiandike jina la mumewe ndiku, shame on u Uwoya!!!!

Nyamgomera Muhozi: jamani kumbe mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu uwoya amesahau diamond alipomla uroda hotelini anafikiri mmewe huyo hakusikia uchungu?

Anonymous: Uwoya bado anayo haki ya kumlinda mumewe hata kama ameharibu mwenyewe, wasanii wa bongo movie pia hawaaminik, na we uwoya utakuja juta siku moja kwa kumtesa shemej yetu, tulia mwanamke.

Hellen Mathias: mhh..shughuli.

Mseli Msuya: Irene pole, ndio maumivu ya mapenzi hayo! ujue na mumeo naye anapata maumivu kwa njia moja ama nyingine akisikia vibweka vyako kama cha juzi wewe na diamond, kimjini tunasema kuwa mpole ngoma droo.

Mjingamjinga Mzee Ali:  mtenda akitendewa upita akilaumu wakati kila ula kuku wa mwezio juwa miguu ukulekea.

Husna Mwalimu: wee uwoya na kule instagram watumia jina la nani vileee! bitch....!!!

Anne Msuya:  mtenda akitendewa upita akilaumu wakati kila ula kuku wa mwezio juwa miguu ukulekea.

Schola Temu: Lucy kama Ndiku kakapenda usivunge Uwoya katutia aibu wanawake wa Bongo tunaonekana hatujui kuthamini ndoa. ustar ni kitu cha kupita uwoya lakini mume huleta familia milele. jipange

Massali Imma: Mfamaji haishi kutapatapa umeshachelwa ndugu

Kiliane Kipande: mtenda hutendw ni zamu yako sasa!

Stellah Mapande: Una haki ya kumlinda mumeo lakini ushachelwa...umemtenda Ndiku wa watu mpaka akazimiaa, zamu yako sasa!

Anonymous:  Wewe ukimuona wa nini wenzio wanajiuliza watampata lini, namshangaa huyo Irene kujifanya kuhoji wakati mwanamme kamshindwa mwenyewe. Lucy mama ikiwezekana kama ni kweli mnadate chukua chombo kimoja hamna kulegeza uzi. Mwanaume anahitaji kuenziwa bibi yamekushinda waachie wenye meno watafune.

Anonymous: Uwoya alikimbilia ndoa wakati damu yake bado inataka kila mwanaume, ndiku usirudi nyuma funga ndoa kabisa na da Lucy ye anajiheshimu na kama sio kweli kuwa na wapenzi basi tafuta hapahapa Tz utampata mwanamke mzuri anayejua kutunza mume.

                                                           Lucy Komba
                                                             Irene Uwoya
 Like our facebook page Swahili World Planet for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, fashions plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

1 comment:

  1. HIVI NI KIASI GANI IRENE ANAZIDI KUJITIA AIBU KUBWA HATA BADO AIBU YA GUMZO LA DIAMOND HALIJAISHA ?? NAOMBA TULIUJUZE HIVI: KUNA BAADHI YA WANAOSEMA KUWA IRENE UWOYA ANAYO HAKI YA KUITETEA NA KUIPIGANIA, SWALI LANGU NI HILI : KWA NINI AITETEE NDOA YAKE BAADA YA KUFANYA MACHAFU TENA NI MARA KWA MARA NA MAGAZETINI NI KILA SIKU ??? SWALI LANGU KUBWA KULIKO YOTE NI HILI: KWA NINI ANAHANGAIKA SANA NA KUWEKA BIFU NA MWANAMKE MWEZIE WAKATI WA KWANZA ALITAKIWA KUWA NA BIFU NA MUMEWE KWA KUWA KAMA NI KWELI HAWAJAACHANA IWEJE MUME AFANYE FILM PILA YA KUMTAARIFU MKEWE? NA KAMA NI KWELI KWAMBA LUCY KOMBA NA NDIKUMANA WANATOKA WOTE SWALI NI HILI: KWA NINI HIYO ISIWE KAMA USHAHIDI KWAMBA NDIKUMANA AMEMCHOKA SANAA IRENE KIASI KIKUBWA HADI AAMUWE KUTOKA NA MTU AMBAYE NDIYE MWALIMU WA SANAA WA MKEWE IRENE UWOYA??? TUTUMIE AKILI SANA BADALA YA MWAZO YETU TU....

    ReplyDelete