SWP: Kuna kipindi ulipumzika kidogo katika kazi zako za filamu lakini hivi umerudi katika game, je mashabiki wako na waandaaji wa filamu wamekupokeaji kwa ujumla?
AMANDA:
Kipindi nimepumzika nashukuru mashabiki wangu walikuwa wanajaribu sana kuniomba nirudi kwenye game na hii inaonyesha ni jinsi gani wana upendo na mimi hivyo bila kubisha nikarudi kwa ajili yao ili kuwaonyesha ni kiasi gani. Nashukuru sana napokea maoni ya wengi wakionyesha ni jinsi gani wamefurahi na mimi nazidi kuwaahidi watazidi kufurahi zaidi ya mwanzo. Ningependa kumalizia kwa kusema kuwa nawapenda sana mashabiki wangu.
SWP: Katika moja ya filamu zako zilizotoka hivi karibuni ni
Nyumba 4 ukiwa na king Majuto na performance yako katika filamu hiyo ni
nzuri, je unazungumziaje kufanya kazi pamoja King Majuto?
AMANDA: Mmmmh....kwanza toka zamani nilikuwa na ndoto za kufanya
kazi na Mzee Majuto na nashukuru Mungu nilifanikiwa hilo....nafurahi sana na
hasa nikiwa naiangalia ile movie huwa kweli naona naweza.
SWP: Kwahiyo bado ungependa kufanya kazi zaidi na King Majuto kuliko wasanii wa kiume wa rika lako?
AMANDA: Napenda kufanya kazi na msanii yeyote because wote tupo katika fani
moja na wote ni ndugu hivyo hata Mzee Majuto akihitaji kufanya kazi na mimi
tena basi nipo tayari.
SWP: Ni kweli umeachana na Bwana Misosi?
AMANDA: Ni kweli mimi na Bwana Misosi tuliachana muda mrefu tu na
hatukuwa tukihitaji kuweka wazi lakini imenibidi kwasababu mashabiki wangu wengi
walikuwa wanasumbua kutaka kujua uhusiano wetu upo au umekufa...ni kweli
tumeachana.
SWP: Lakini kutokana na alivyonukuliwa na media inaonyesha
Bwana misosi hakutarajia media zijue kuwa mmeachana na inaonyesha kama
bado anakupenda ila wewe hutaki?
AMANDA: Kwa upande wake siwezi kumsemea moyo wake ila kwa upande
wangu sipo tayari na wala sifikirii kurudiana nae....tumebaki marafiki wa
kawaida tu.
SWP: Sasa hupati usumbufu wowote kutoka kwa wanaume ukifikiria wewe ni mwanamke mrembo, uliyejaaliwa mvuto na maarufu pia?
AMANDA: Ha ha ha haaa hiyo ni kawaida ila najiheshimu na naheshimu watu wote na kikubwa ninaye mtu wangu ambae tunaheshimiana sana.
SWP; Ni muigizaji gani wa kike nchini unakubali sana kazi au kipaji chake na kwanini yeye?
AMANDA: Namkubali sana Riyama Ally..yupo makini sana na kazi na anajua nini anafanya.
SWP: Wewe ni mmoja wa mastaa wachache wa filamu ambao huwa unajumuika na mashabiki wako moja kwa moja kupitia mitandao ya kijamii(social networks) kama
vile Facebook na hata kuelezea hisia zako juu ya kitu flani wakati mwingine,
hivyo unafikiri mastaa wengine ni muhimu kuwa karibu na mashabiki wao
kama unavyofanya wewe kupitia social networks?
AMANDA: Mimi binafsi napenda sana kuwa karibu na mashabiki wangu kwasababu
nakuwa najua kwa urahisi nini wanapenda na nini wanachukia. Pia mara
nyingi wengi wao huwa wananipa ushauri na naupokea kwa mikono
miwili hivyo nawashauri wasanii wenzangu wawe karibu na mashabiki sababu kuna
faida............maringo hayasaidii.
SWP: Kwasasa una-shoot filamu gani na labda nyingine ambazo zimeshakamilika zinatarajiwa kuingia sokoni muda si mrefu?
AMANDA: Kwa mwezi huu wa Ramadhani niligoma kupokea kazi yoyote hivyo
mpaka mwezi ukiisha natakiwa kuingia location ku-shoot movie mpya pia
nitaizungumzia nikianza. Lost Future na Panga La Moto zimeshakamilika na nina imani zitakuwa ni filamu bora na zitakazopendwa sana na mashabiki.
SWP: Ni kitu gani huwa kinakukera katika tasnia ya filamu na ungependa kisiwepo?
AMANDA: Sipendi wasanii wanavyobaguana hilo ndio kubwa
linalonikera, wasanii tupendane kwa sababu wote tupo katika fani moja... i mean kazi
moja so tupendane because wote ni ndugu.
Like our facebook page Swahili World Planet for more updates about Swahili movies' latest news, gossip, celebrities, features, fashions plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
No comments:
Post a Comment