Wapo wengine wachache sana lakini Nisha nimemchukulia kama mfano mzuri kwa ninavyomuana. Baadhi ya waigizaji wanapoalikwa kwenye media utawakuta wakijadili/kuzungumzia na kuulizwa kuhusu skendo zao kwa kiasi kikubwa au maisha yao binafsi bila hata kupigia promo filamu zao mpya. Waandaji na wasambazaji wa filamu husika mara nyingi na ni lazima wawe na team au mipango ya kuipigia promo ya kutosha kazi mpya kabla ya kutoka na hata miezi kadhaa baada ya kutoka ili kazi ijulikane kwa wadau na kufanya vizuri sokoni hapa hata bajeti ya promo na marketing ni lazima itengwe. Kitendo hiki pia kitaanza kuondoa ile kasumba ya kuangalia jina la star ili kununua kazi kwani promo ikishapigwa ya kutosha ni rahisi walaji kununua kazi kuliko kutoipigia promo kabisa. Suala hili kwa kiasi kikubwa linawahusu wasambazaji, waandaaji na hata waigizaji wa filamu husika ni lazima wafanye juu chini kuipigia promo kazi mpya katika social media kama twitter, Facebook, kwenye vipindi vya Tv, Radio, billboards, posters na mahojiano magazetini ni lazima wafanye hivyo ndiyo inavyokuwa na sio kuwa muigizaji akishamaliza shooting ya filamu basi ndiyo kamaliza kila kitu haimuhusu tena huko ni kukosea.
Ni wazi kuwa wasanii wengi nchini bado hawajajua umuhimu wa social media katika kutangaza kazi zao na ndiyo maana kuna wasanii kibao hawapo mitandaoni na hata wale waliopo hawafanyi juhudi zinazotakiwa katika kutangaza kazi zao. Utakuta msanii ana zaidi ya Likes au Followers 5000 lakini miezi inapita hajatangaza kazi zake mpya hapo licha ya kwamba zinaingia sokoni kila wiki. Tubadilike wadau kwa kutumia fursa zilizopo. Elimu ya filamu pia ni muhimu sana.
No comments:
Post a Comment