Saturday, July 13, 2013

HONGERA SALMA JABU(NISHA), WASANII WENGINE IGENI MFANO.

Miezi ya hivi karibuni nimekuwa nikifurahia kitu kimoja kutoka kwa actress/producer Salma Jabu(Nisha) ambaye anamiliki kampuni ya kutengeneza filamu ya Nisha's Film Production. Ni hivi Nisha amekuwa mstari wa mbele kutangaza kazi zake mpya yaani filamu zake mpya hasa alizotengeneza mwenyewe. Amekuwa akitangaza sana kwenye media kama vile Tv na social networks na hata blogs kuonyesha kuwa muigizaji huyu anaelekea kule film industry inapotaka hasa katika suala la marketing of films. Jana pia alikuwa katika kipindi cha Hot Mix kinachorushwa Channel 5 na nilifurahia alipokuwa anaipigia promotion ya kutosha filamu yake mpya ya Tikisa. Hii ndivyo inavyokuwa hasa Hollywood na Bollywood filamu mpya ni lazima ifanyiwe marketing ya kutosha katika kila nafasi inayopatikana na wakati mwingine sio lazima mpaka wahusika wa kipindi wakuite bali unaweza zungumza nao hii ndiyo inavyokuwa. Hata hivyo cha kusikitisha waigizaji wetu wengi, waandaaji wa filamu na hata wasambazaji bado hawajaanza kutumia fursa kama hizi vizuri katika vipindi vya kawaida vinavyohusu sanaa ingawa pia mizengwe ipo kwa baadhi ya host wa vipindi hivyo kutaka rushwa lakini mabadiliko ni haya tunayoanza kuyaona kupitia watu kama Nisha.

Wapo wengine wachache sana lakini Nisha nimemchukulia kama mfano mzuri kwa ninavyomuana. Baadhi ya waigizaji wanapoalikwa kwenye media utawakuta wakijadili/kuzungumzia na kuulizwa kuhusu skendo zao kwa kiasi kikubwa au maisha yao binafsi bila hata kupigia promo filamu zao mpya. Waandaji na wasambazaji wa filamu husika mara nyingi na ni lazima wawe na team au mipango ya kuipigia promo ya kutosha kazi mpya kabla ya kutoka na hata miezi kadhaa baada ya kutoka ili kazi ijulikane kwa wadau na kufanya vizuri sokoni hapa hata bajeti ya promo na marketing ni lazima itengwe. Kitendo hiki pia kitaanza kuondoa ile kasumba ya kuangalia jina la star ili kununua kazi kwani promo ikishapigwa ya kutosha ni rahisi walaji kununua kazi kuliko kutoipigia promo kabisa. Suala hili kwa kiasi kikubwa linawahusu wasambazaji, waandaaji na hata waigizaji wa filamu husika ni lazima wafanye juu chini kuipigia promo kazi mpya katika social media kama twitter, Facebook, kwenye vipindi vya Tv, Radio, billboards, posters na mahojiano magazetini ni lazima wafanye hivyo ndiyo inavyokuwa na sio kuwa muigizaji akishamaliza shooting ya filamu basi ndiyo kamaliza kila kitu haimuhusu tena huko ni kukosea.

Ni wazi kuwa wasanii wengi nchini bado hawajajua umuhimu wa social media katika kutangaza kazi zao na ndiyo maana kuna wasanii kibao hawapo mitandaoni na hata wale waliopo hawafanyi juhudi zinazotakiwa katika kutangaza kazi zao. Utakuta msanii ana zaidi ya Likes au Followers 5000 lakini miezi inapita hajatangaza kazi zake mpya hapo licha ya kwamba zinaingia sokoni kila wiki. Tubadilike wadau kwa kutumia fursa zilizopo. Elimu ya filamu pia ni muhimu sana.

Filamu ya Tikisa imeingia sokoni jana ijumaa hivyo jipatie nakala yako halisi sasa

No comments:

Post a Comment