Muigizaji wa filamu za Comedy Swahiliwood Nicolaus Ngoda maarufu kama Ukwa wa Bongo kwasasa hayupo chini ya kampuni ya Bornagain Film Production ambayo ndiyo imemtoa kwenye game la movies na kujulikana kwa mashabiki wengi wa filamu. Kampuni hiyo inamilikiwa na Emanuel Myamba(Pastor Myamba). Akichonga na Swahiliworldplanet muigizaji huyo machachari amesema kuwa amejitoa mwenyewe baada ya kutotimiziana mambo flani na kampuni hiyo katika mkataba wao wa awali. Ameendelea kusema kuwa hawana ugomvi bali kila mtu ana amani na mwenzake na kwasasa yupo huru kwa hiyo muandaaji yeyote yule anaweza kufanya kazi nae wakikubaliana kikazi. Pia amesema kuwa anaweza kutumiwa tena na kampuni hiyo kama msanii wa kawaida na siyo kutoka kwenye label au mkataba hivyo atakuwa huru kufanya kazi zake mwenyewe pia.
Muigizaji huyo pamoja na mwenzake Meya Shabani(Aki wa Bongo) wameigiza filamu nyingi chini ya kampuni hiyo na wasanii wengine wenye majina akiwemo Rose Ndauka. Huwa wanafananishwa na Aki na Ukwa wa Nigeria.
No comments:
Post a Comment