Thursday, June 6, 2013

SOLANGE DAVID KUANDIKA STORY YA MAISHA YAKE KWA AJILI YA KUCHEZWA FILAMU.

Solange David mmoja wa waigizaji wa filamu za kiswahili nchini Denmark ana mpango wa kuyaweka maisha yake katika filamu kwa kuandika story ya maisha yake kutoka kote alikopitia mpaka kufikia alipo sasa. Solange ambaye ni mama wa watoto wawili mmoja wa kike na mwingine wa kiume amesema kuwa hadithi ikishakamilika wataicheza filamu na wasanii wenzake wa filamu za kiswahili nchini humo ili kufikisha ujumbe kwa jamii kwani anaamini story ya maisha yake huweza kutoa funzo kwa watu wengine. Muigizaji huyo aliongeza kuwa waigizaji wenzake nchini humo wazidi kupendana ili kufikia malengo na kupata maendeleo zaidi na kuacha chuki ambazo hazimfikishi mtu popote kimaendeleo. Muigizaji huyo ni mtoto wa tatu katika familia yao huku akiwa na ndugu zake wengine saba wanaomfuatia. alizaliwa Congo na kukulia Kigoma Tanzania na kwasasa ni mwanafunzi wa chuo kikuu nchini humo.


No comments:

Post a Comment