Thursday, June 6, 2013

KING MAJUTO KUWA MUONGOZAJI UZINDUZI MPYA WA ZUKU SWAHILI MOVIES JUMAMOSI HII ARUSHA.

Baada ya Africa Magic Swahili katika kuanza kuonyesha Swahili movies sasa ni zamu ya Zuku Swahili movies ambao watafanya uzinduzi wao mpya tarehe 8 Jumamosi hii Katika hoteli ya Naura Spirings, Arusha, Tanzania. Shughuli nzima itaanza saa 12:00 jioni, vazi maalum ni vazi la kiafrika, chakula kitakuwa cha kiafrika na burudani nyingine kibao kama vile muziki. Wahudhuriaji ni wale ambao wamearifiwa au kupewa mwaliko maalum huku mwongozaji wa event hiyo akiwa muigizaji maarufu Africa mashariki na kati King Majuto kama anavyotambulika kwa mashabiki wengi wa filamu. Tunaamini uanzishwaji wa vituo vingi vya Tv kwa ajili ya filamu za kiswahili utaleta ushindani wa soko na kuinua pato la msanii baadaye licha ya kwamba kwasasa bado hali si nzuri katika malipo ya wasanii, pia ushindani huu utasaidia kutangaza zaidi filamu za Swahiliwood miaka michache ijayo. Kila la kheri Zuku Swahili Movies.


No comments:

Post a Comment