Sunday, June 9, 2013

LUCY KOMBA AJIFUNZA KARATE ILI KUWAFUNZA ADABU WANAUME WAKOROFI, KUBADILISHA MUELEKEO WA FILAMU ZAKE PIA.

Actress maarufu Lucy Komba ameanza kufanya mazoezi ya karate katika viwanja vya Gymkhana kwa lengo la kujiweka fit kwa lengo la kukabiliana na wanaume wanyanyasaji hasa kwa mtoto wa kike. Akizungumza na gazeti la Mwananchi muigizaji huyo anayezidi kukuza soko la filamu zake nje ya nchi alisema lengo jingine la kuanza kufanya mazoezi ya karate ni kutaka kubadilisha muelekeo wa filamu zilizozoeleka sasa, hivyo tarajia kumuona the talented actress katika filamu za kimapigano pia. Na kama wewe ni mwanaume uliyezoea kunyanyasa wanawake basi huu ndiyo mwisho wake maana Lucy hataki mchezo kwasasa.
"“Kwanza mchezo wa karate nilikuwa naupenda sana tangu nikiwa mdogo, najiweka vizuri ili pia kupambana na masuala ya unyanyasaji hasa kwa mtoto wa kike, ambayo yamezidi. Wanaume wakorofi hawatanisumbua,” alifunguka muigizaji huyo aliyewaibua mastaa wengi wanaotamba sasa.

                                                  Lucy Komba


No comments:

Post a Comment