Mwanamuziki TID nae amejitoa kwenye show ya miaka 13 ya Lady Jaydee na watu kumshambulia vibaya kwa kitendo chake hicho kuwa hana utu, ujasiri wala sababu ya msingi. watu hao pia wamesema wanamuziki wa Tanzania hawana umoja ndiyo maana wataendelea kunyonywa siku zote wakati Jaydee anapaswa kupewa sapoti kwa kuwa alichokisema na kukiamini tayari wengine walishakisema kama vile Anti-virus na hata wasanii wengine wanaokuja bado wataendelea kukisema kama watakosa umoja na kusapotiana bila hofu. TID aliandika hivi FB "“Three reason why i can’t do lady JIDE SHOW ………….No.1 I have better
contract pays me better than.No.2 I really don’t want to be between
anybody’s conflict ya kwangu yananishinda naona nieupushe shari…No.3
nataka kuoa muda wangu ndo huu ……………kama nimekukosea captein na madame
kazeni but I have been thru same shit.”. Watu walimshambulia kuanzia hapo na kwenye blogs na mitandao mingine wakionekana kuwa upande wa Jaydee na kumuona TID ni mmoja wa wasaliti wa maendeleo ya muziki nchini. Tayari Linah, Barnaba na Matonya pia wamejitoa huku fans wengi wakimpa moyo Jaydee kuwa mungu na wao wapo upande wake, Inadaiwa wanamuziki hao wamejitoa kwa shinikizo la Ruge na Kusaga ambao wana tofauti na Jaydee mpaka kufikia kumfungulia kesi mahakamani. Ili kusoma baadhi ya maoni ya watu kuhusu TID ingia hapa www.bongoclantz.com
No comments:
Post a Comment