Waziri Kivuli wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Joseph
Mbilinyi akisoma hutuba ya kambi ya upinzani hivi punde amesema kwamba
baadhi ya vyombo vya habari vikiwamo vituo vya redio vimekuwa
vikiwanyonya wasanii nchini na kusababisha kuwa maskini.
Joseph
Mbilinyi maarufu Sugu amesema bungeni kwamba hivi sasa kuna mgogoro
mkubwa kati ya Lady Jay Dee na Radio Clouds FM, lakini serikali imekaa
kimya mpaka sasa.
"Serikali imekaa kimya haitatui matatizo ya
wasanii, hivi leo Clouds FM haipigi muziki wa Lady Jay Dee, tunakwenda
wapi, chama cha wasanii ambacho ni halali
kimetaifishwa na kuundwa kampuni ya kusimamia shughuli za wasanii, lakini kwa malengo ya kuwanyonya," amesema Sugu.
Kutokana
na mgogoro unaoendelea kati ya Lad Jaydee na Clouds FM, Sugu ambaye ni
Mbunge wa Mbeya Mjini amewataka wasanii Tanzania kuacha uwoga na kutetea
haki zao.
Pia kupitia hutuba hiyo Sugu ameitaka serikali
kuchukua hatua ya kuwatetea wasanii na iache kuwatumia kwa maslahi yao
binafsi. Sugu akihitimisha hutuba yake, amelieleza Bunge kwamba Lady Jay
Dee anatimiza miaka 13 tangu aanze muziki na kwamba atafanya tamasha
kubwa jijini Dar es Salaam ambalo litafanyika Mei 31, mwaka huu jijini
Dar es Salaam.
"Kabla sijaitimisha napenda kuwaambia kwamba Jay
Dee atafanya tamasha la kusherekea miaka 13 tangu aanze muziki hivyo
dada napenda kukuhakikishia kwamba tutakuwa pamoja pale Dar es Salaam,"
Sugu amesema hivi punde bungeni.
Sugu amemaliza kusoma hutuba ya kambi ya upinzani na sasa wabunge wameanza kuchangia.
credit www.habarimasai.com
No comments:
Post a Comment