Wednesday, May 1, 2013

LADY JAYDEE: HATA NIKIFA CLOUDS FM MSIPIGE NYIMBO ZANGU WALA KUNIONGELEA RADIONI.

Lady Jay leo amefunguka kuliko kawaida katika bifu lake na Clouds fm chini ya Mr. Kusaga na Ruge. Jaydee amesema kuwa hata kama akifa asingependa nyimbo zake zipigwe katika radio hiyo wala kutamka chochote kuhusu yeye kwa kuwa ni wanafiki na watu wabaya wanaotaka wampoteze kisanii. Amesema wengine wanamuona yeye ni mnafiki baada ya kubebwa na radio hiyo kwa miaka kumi lakini mwenyewe amekanusha na kusema kuwa mambo yalianza kwenda vibaya tangu mwaka 2003 alipojitoa Smooth Vibes baada ya  albamu yake ya Binti chini ya kampuni ya Smooth Vibes chini ya Ruge. ilikusoma alichoandika mwanamuziki huyo maarufu Afrika mashariki ingia hapa www.ladyjaydee.blogspot.com


No comments:

Post a Comment