DIRECTOR: Rashid Mrutu
CAST: Janeth Lameck, Ruth Suka, Zuberi Mohamed, Hamis Korongo, Mohamed Fungafunga.
RATING: 3/5
Filamu nyingi za Tanzania huharibiwa kwa waandaaji kulazimisha kuwa na part 1 na part 2 pasipo mantiki yoyote kutoka katika story husika. Moja ya filamu hizo ni filamu mpya ya "Binti Kidawa", wazo la hadithi yake ni zuri na limebeba ujumbe mzuri lakini screenplay haijaandikwa vizuri kwa kuirefusha pasipo maana ya msingi. Kama screenwriter angeiandika vizuri na hii filamu kuwa na sehemu moja tu bila kulazimisha part 2 ingekuwa ni filamu nzuri sana. Muongozaji wa hii filamu ambaye ni Rashid Mrutu pia hakufanya kazi vizuri katika hii filamu huku mhusika mkuu Janeth Lameck(Kidawa) akifunikwa na waigizaji wengi wasaidizi akiwemo Bi. Stara wa Kaole na Ummy wa Mambo hayo waliokuwa poa sana katika characters zao. Nafikiri huu ni muda sasa wa waandishi na screenwriters kufanya kazi nzuri ili kuwa na filamu nzuri na sio kulazimisha part one na part 2 pasipo kuwa na mantiki yoyote ya kufanya hivyo. Kizuri katika hii filamu ni location walijitahidi sana zilikuwa nzuri, waigizaji wengi pia walicheza vizuri na pia story kuonyesha baadhi ya mila na tamaduni za kiafrika yaani jando na unyago kama vile Bi. Stara alivyokuwa akimfunda Binti Kidawa ilitoa nguvu zaidi katika story. Bi Stara ndiye anayekuvutia zaidi katika hii filamu licha ya mwandishi kutompa nafasi kubwa huku Ummy wa Mambo hayo naye akitukumbusha enzi hizo. Mainda, Niva na Mohamed Fungafunga Jengua walikuwa poa pia katika nafasi zao.
Binti Kidawa ni filamu inayoelezea story ya Binti mmoja Janeth Lameck akiwa na ndoto za kusoma lakini anapitia misukosuko mingi ikiwemo kulazimishwa kuolewa na baba yake mzazi asiyeweza kutunza familia yake(Jengua), na baadaye kubakwa na baba yake wa kambo(Mzee Korongo) na kupata mimba hivyo kujifungua akiwa bado mdogo na kumtelekeza mwanae. Analazimika kumuua mama yake mzazi na baba yake wa kambo kwa kuchoma nyumba moto wakiwa ndani kutokana na kubakwa na baba wa kambo huku mama yake akiwa hasikii chochote kwa mpenzi wake huyo mnyanyasaji.
Itafute uiangalie kama bado kuiona unaweza kufurahia mikikimikiki anayopitia Kidawa.
No comments:
Post a Comment