Tuesday, April 16, 2013

ACTRESS HALIMA YAHAYA(DAVINA) AJIFUNGUA BABY BOY.

Actress maarufu wa Swahiliwood Halima Yahaya(Davina) amejifungua salama mtoto wa kiume jana na wote mama na mtoto wanaendelea vizuri kwa mujibu wa chanzo chetu. mastaa kibao wa muziki na filamu walienda kumpongeza actress huyo aliyeanzia uigizaji katika kundi la Kaole Sanaa Group na pia ameshacheza filamu nyingi na mastaa wenzake kibao wakiwemo Jacob Stephen na Single Mtambalike(Rich). Tunawatakia afya njema mama na mtoto huyo na kama atakuwa amerithi kipaji cha mama yake basi miaka ijayo mtoto huyo anatarajiwa kuonyesha cheche zake Swahiliwood.



No comments:

Post a Comment