Wednesday, March 20, 2013

TANZANIAN ACTORS WAPOKELEWA KISHUJAA RWANDA. HII IWE FUNZO KWA SERIKALI YETU.

Serikali ya Tanzania haifanyi juhudi za dhati kuisapoti tasnia ya filamu nchini licha ya filamu za Tanzania na actors wake kupendwa sana nchi jirani kiasi cha mashabiki wa nchi hizo kupagawa wanapowaona mastaa wa filamu za kitanzania. Serikali iache siasa badala yake ichukue hatua kwa vitendo katika kusaidia  usambazaji, hatimiliki na kuruhusu taasisi na maeneo ya serikali kutumika katika films za Swahihiliwood. Hivi karibuni. Swahiliwood actors Vicent Kigosi( Ray), Irene Uwoya, king Majuto, na Jacob Stephen walialikwa kama watu maarufu katika tuzo za filamu nchini Rwanda na kupokelewa kishujaa kiasi cha fans kupagawa na baadhi kulia kwa kutoamini. Pia King Majuto alipoingia ukumbi mzima ulisimama kuonyesha heshima na kwa jinsi gani kazi zake zinakubalika lakini cha kusikitisha wasanii hao nyumbani kwao(Tanzania)  hakuna tuzo za filamu kitu ambacho ni aibu kwa tasnia hii na serikali kwa ujumla  kwa tasnia yenye zaidi ya miaka kumi sasa.

 Rwanda yenyewe inaangalia Tanzanian film industry kama their inspiration na wao wameanza juzi tu lakini tayari wana tuzo zao. BASATA nayo inaonekana kusimamia na kuweka vigezo vigumu kwa wenye pesa tu kuanzisha tuzo na siyo wadau wa kweli wenye uchungu na Tasnia hii. Kupata kibali ni issue tena utoe pesa zaidi ya milioni 1.5. BASATA yenyewe imeshindwa kuiga nchi nyingine kwa kuwa na tuzo zake za kuwatukuza wasanii wa nchini kila mwaka kama zilivyo nchi nyingine kama India yenye tuzo za National Awards ambazo ni za serikali na hutolewa kila mwaka huku kukiwa na tuzo nyingine kibao. BASATA wapo ofisini tu wakingoja tasnia ikuwe lakini wao hawachukui hatua za dhati kuindeleza tasnia hii. Serikali pia inatakiwa ifanye namna hata kuzungumza na mabenki nchini ili watengenezaji wa filamu wenye vigezo wapate mikopo kwa masharti nafuu. Angalia picha jinsi wasanii wetu walivyoonekana kama mashujaa huko Rwanda..........

King Majuto alipoingia ukumbi mzima ulisimama kuonyesha heshima kwa msanii huyo
                             Shabiki wa kike alilia kwa kumuona Ray live.

                                                images by bongo5

No comments:

Post a Comment