Tuesday, March 26, 2013

HONGERA SANA WEMA SEPETU KWA KUWA NA WEMA KAMA JINA LAKO LILIVYO.

Kwanza niseme kuwa licha ya actress and former Miss Tanzania Wema Sepetu kuandamwa na skendo kadhaa lakini bado Wema ana sifa za kuitwa star halisi hii ni kwasababu kwa asilimia kubwa Wema anaishi yeye kama yeye na siyo mtu wa kuficha maisha yake halisi, wapo celebs walio wachafu but wanaonekana wasafi kwa kuwa wanajificha sana. Wema mara nyingi ni mtu wa kujitoa kusaidia pale alipo na uwezo huo kama tulivyoona jana alipotoa zaidi ya shilingi mil 10 kama faini ya actress mwenzake Kajala Masanja. Ndiyo wapo mastaa wasio na skendo but huwa hatuwaoni wakisaidia wenzao au jamii yenye matatizo licha ya mastaa hao kuwa na uwezo wa kufanya hivyo. Hakika Wema anahitaji pongezi zaidi ya mara moja. Wema mwenyewe alikaririwa akisema kuwa alimsaidia actress mwenzake Kajala kwa kuwa anajua hata yeye ipo siku anaweza kupata tatizo hivyo kuhitaji msaada wa wengine kitu kinachoonyesha kuwa Wema anajua nini maana ya maisha na namna ya kuishi vizuri na jamii inayomzunguka  kwa kusaidiana katika shida na raha. Wema alisema..."Unajua matatizo kaumbiwa binadamu na yakimfika mwenzako usifurahie bali sikitika pamoja nae lakini kama unaweza kumsaidia ni vizuri ukamsaidia kama ukishindwa sikitika pamoja nae na ndio maana nimefanya yote kwa pamoja kusikitika pamoja nae na kumsaidia pia"

Wasanii endeleeni na moyo huu wa kusiadiana katika shida na raha Wema, Dr Cheni, Jackline Wolper na wengineo wachache wakiwa mfano mzuri kwa kujitoa kusaidia. Pia hii iwe katika Tanzanian music na pia katika Tanzanian fashion industry watu kusaidiana kwenye shida na raha. Hongera tena Wema Sepetu kwa kuwa na WEMA na moyo wa huruma kama jina lako lilivyo WEMA Sepetu, Mungu akuzidishie zaidi ya ulichotoa na pia akupe maisha marefu zaidi.

Actress Wema Sepetu, Kajala Masanja and Dr. Cheni akionekana kwa nyuma.
                                                                   Wema Sepetu






No comments:

Post a Comment