Tuesday, March 26, 2013

DAXX: MODELS WENGI TANZANIA NI WAOGA NA HAWAKO SERIOUS.

Tanzanian international model based in South Africa Daxx Hans amesema kuwa models wengi wa Tanzania ni waoga wa kuthubutu, hawako serious na kazi ya modelling bali wanafanya kama starehe ndiyo maana wanashindwa kuchomoka kimataifa licha ya wengi wao kuwa na vigezo vya modelling. Daxx ambaye anafanya vizuri kwa sasa S.Afrika aliyasema hayo alipoulizwa na SWP kuwa anafikiri nini kinakwamisha models wengi wa Tanzania kufanya kazi internationally, Daxx alisema "wat i can say is,models wengi wa bongo ni waoga katika kujaribu,then wengi they r not seriously about wat thy r doing in fashion kwa ujumla!..wanachotakiwa kufanya ni kupanua fikra zao na kuheshimu kile wakifanyacho,na kugeuza kuwa kazi na si starehe kama wengi wanavyohisi"

Daxx pia alisema yeye anafanya fresh huko S.Afrika now because anaheshimu kazi yake, ndoto na mawazo yake pia ndiyo maana yupo alipo sasa. Pia baadhi ya watu huko S.Afrika hawaamini kama Daxx ni mtanzania badala yake wanadhani kuwa anatokea Nigeria au U.S.A kwa kuwa hakuna model wa kiume from Tanzania aliyewahi kufanya kazi internationally. "am doing good because naheshimu ninachofanya,na pia naheshimu ndoto na mawazo yangu,and also siogopi kufanya kitu nikitakacho...Huku wanakataa kama mimi ni Mtanzania,wanasema natoka Nigeria or USA,so do u think why?coz hakuna models wa kiume kutoka Tanzania anayefanya au aliyewahi kufanya modeling nje,thats y hawataki kuamini kabisa kama mimi ni mtanzania,ila nw wanaamini coz i show them my ID"

Hayo ndiyo aliyosema Daxx na kuna msemo usemao "kufanikiwa ni kuthubutu" hivyo bila kuthubutu models wengi Tz hawawezi kuwika internationally.


No comments:

Post a Comment