Friday, March 29, 2013

DIAMOND AMJENGEA MAMA YAKE NYUMBA YA MIL.260, INA UWANJA WA BASKETBALL, SWIMMING POOL, STUDIO NA GYM.

Diamond Platinumz anaonekana kumpenda sana mama yake huku mara nyingi akikaririwa akisema kuwa mama yake huyo ana mchango mkubwa sana katika mafanikio yake kisanaa. Habari ni kuwa the polular singer amemjengea nyumba  mama yake Sanura Kassim(Sandrah). Nyumba hiyo ambayo ipo Tegeta ina thamani ya shilingi mil. 260 za kibongo ikiwa kama zawadi kwa mama yake. Nyumaba hiyo ina vyumba vinne vya kulala ambavyo vyote ni self contained, studio ya kisasa ya muziki, eneo ambalo limetengwa maalum kwa ajili ya swimming pool la kisasa, uwanja wa basketball na gym. Nyumba hiyo inatarajiwa kukamilika september mwaka huu. Diamond pia alimnunulia mama yake gari aina ya Alteza  Akiongea na mtandao wa globalpublishers Diamond alisema “Mama yangu ndiyo kila kitu kwangu, mara ya kwanza nilimnunulia gari aina ya Toyota Alteeza nikaona haitoshi, nikaamua kumjengea hii nyumba ambayo itakuwa kama urithi wake hata nikifa leo”.  

Ukiachana na ukubwa wa nyumba hiyo, uwanja ambao ameuzungushia uzio wa ukuta kuna nyumba nyingine ndogondogo tatu ambazo kwa mujibu wa Diamond zitakuwa zikipangishwa.Kwa sasa star huyo anakaa nyumbani kwake Sinza.

Hongera sana Diamond kwa kumkumbuka mzazi wako na pia kwa kufanya mambo ya kimaendeleo tofauti na wengine wanaondekeza starehe bila mpango. .

Hii ndiyo nyumba yenyewe ikiendelea kujengwa, na linaloonekana ni gari yake.
                                      Diamond akiwa nyumbani kwake Sinza

No comments:

Post a Comment