Pages

Friday, February 1, 2013

WEMA SEPETU ACHUKUA FORM KUSHIRIKI BIG BROTHER AFRICA 2013

Taarifa zinadai kuwa actress Wema Sepetu amekwenda ofisi za MultiChoice na kuchukua form kwa ajili ya mchakato wa awali wa kutafuta mwakilishi wa shindano maarufu la Big Brother Africa 2013.Baadhi ya watu wanadai Wema ana vigezo vyote vya kuwa mwakilishi ukiachilia mbali skendo zake zinazoripotiwa mara kwa mara magazetini, wakati wengine wanasema hafai ataenda kutuaibisha na skendo zake na wanasema aende mtu ambaye siyo star ili kuzidi kuongeza idadi ya mastaa nchini.Swahiliworldplanet lilimuuliza meneja wa Wema ambaye ni Martin Kadinda kama ni kweli Wema amechukua form ya kushiriki Big brother Africa 2013 katika ofisi za Multichoice, Martin alijibu kwa ufupi"Hapana hajachukua form", Martin alipoulizwa tena kama Wema anao mpango wa kuchukua form au hana mpango huo kabisa? Martin hakujibu mpaka tunaandika habari hii. muigizaji mmoja maarufu alipoulizwa na swahiliworldplanet kama ana taarifa za wema kuchukua form ili kushiriki BBA 2013 alisema "Mh sijui, inawezekana bt akipata hiyo chance tusishangae akirudi mjamzito au akiwa na mtoto".mdau mmoja wa shindano hilo alipoulizwa maoni yake kuhusu Wema kama anafaa au Lah alisema " Mi namkubali Wema kwa kuwa hafichi mambo yake na shindano lile ndiyo mwake,kama Wema akiwa mwakilishi ni lazima ninunue king'amuzi cha DSTV ili nishuhudie vituko vya Wema live. Habari ndiyo hiyo.......let's wait n see

2 comments:

  1. safii,anafaa bana mwacheni akajiachie huko....

    ReplyDelete
  2. Nafikiri tuache kufikiria mambo potofu juu ya Wema sepetu. KIMSINGI PAMOJA NA SKENDO ALIZONAZO let her go there and apply what she has to get the prize. Big brother africa ni game wakati mwingine game inakufanya ufanye mambo fulani ili kuhakikisha una wini.Siamini kama kina Barotel, Ferdinand wana tabia mbaya kiivyo uwanjani ila game linawafanya wafanye vile si kwa sababu wanapenda, LET HER GO BWANA, SHE IS CONFIDENT, BEAUTIFUL, AWESOME, VERY ATTRACTIVE, WHO KNOWS ANAWEZA AKASHINDA. Na kama ni kuwashauri multchoice TANZANIA wema is the best take her.

    ReplyDelete