Pages

Friday, February 1, 2013

MTANZANIA AWAPAGAWISHA NICK MINAJ NA MARIAH CAREY AMERICAN IDOL 2013

Kijana mwenye asili ya Afrika mashariki kutoka kwa mama mtanzania na baba mkenya amewakosha majaji wa American Idol 2013 wakiwemo Nick Minaj, Mariah Carey na Randy Jackson kwa kuonyesha uwezo mkubwa wa kuimba hivyo kuvuka kutoka hatua ya awali na kuingia hatua nyingine ya shindano hilo maarufu duniani ambao limeshatoa mastaa kibao.Kijana huyo anaitwa Sanni M'mairura na anaweza kuongea lugha ya kiswahili .Majaji hao walimuuliza kama anaweza kuongea lugha ya wazazi wake/yenye asili ya kwao, kwa kujiamini Sanni alijibu "Ndiyo naweza kuongea kiswahili" kabla ya kuanza kuimba wimbo wake. Baada ya kumaliza kuimba majaji hao wakiwemo Nick Minaj na Mariah Carey walionekana kukubali uwezo wake na hivyo kumpa tiketi ya kwenda Hollywood kukutana na washiriki wenzake kutoka majiji tofauti ya marekani ambako watakuwa kambini,mcheki jamaa huyu anayeelekea kuwa superstar kutoka Afrika mashariki.


No comments:

Post a Comment