Pages

Thursday, January 31, 2013

BASATA IJITAZAME UPYA ILI KUWA NA TASWIRA HALISI KAMA CHOMBO CHA KUKUZA SANAA NCHINI

Baraza la sanaa la taifa BASATA licha ya kuwa na kauli mbiu ya kukuza, kuendeleza na kudumisha sanaa na utamaduni nchini lakini ukiangalia hali inaonekana kuwa tofauti na kauli mbiu yake hiyo. Mpaka sasa hakuna tuzo za filamu na hata zile za muziki ni za aina moja tu na siyo kuwa hakuna wadau ambao wanaojitokeza ili kuanzisha tuzo za aina mbalimbali wapo sana hata BASATA yenyewe inajua maana wamekwenda hapo na bado wanakwenda lakini mara zote tuzo hizo hazifanyiki na wahusika wakiulizwa wanasema BASATA haileweki.kwanza kabisa sababu zikiwa eti kuna ambao wameshasajili tuzo hizo kwa hiyo mwingine hawezi kusajiliwa kwa kuwa categories za tuzo zitakuwa zile zile!.
Hivi BASATA haijifunzi kutoka mataifa mengine yaliyoendelea katika sanaa ziwe za filamu, muziki, fashion na nyinginezo kwa nchi hizo kuwa na tuzo hata zaidi ya 10 katika fani ya aina moja pekee mfano filamu au muziki! niseme kuwa tuzo hazina sana haki miliki kwa kuwa huku ni kuua sanaa ya taifa zima, kinachotakiwa ni tuzo kuwa tofauti katika uandaaji wa tamasha na maeneo machache sana lakini categories nyingi za tuzo zinakuwa zile zile tu zinazobadilika ni categories chache sana ambazo hazina uzito sana, lengo ni kuwapongeza wasanii waliofanya vizuri. Tuzo hazina ubunifu wa kisanaa kiasi cha kuwekewa haki miliki kama ilivyo katika filamu au muziki kwa muandishi kuandika story, mashairi,sauti na nyinginezo.yaani bila sanaa hizi hakuna tuzo na hili linaeleweka kwa mabingwa wote wa sanaa duniani na ndiyo maana katika tuzo ziwe Hollywood au Bollywood na kwingineko kinachobadilika katika tuzo ni majina ya tuzo tu na vitu vichache lakini categories muhimu hubaki kuwa zile zile katika tuzo tofauti na washindi wakitofautiana au kuwa wale wale kutokana na majaji na kura za washindi kutofautiana uwezo na hata uchaguzi wa washindi.
Tuangalie mifano hii huko Hollywood kuna tuzo kibao mfano Oscar, Golden Globe Awards, People's Choice Awards,Critics Choice Awards na nyinginezo. Tuangalie Bollywood mfano zipo tuzo za Filmfare Awards, National Awards,Stardust Awards,Zee cine Awards,International Indian Film Academy Awards(IIFA AWARDS),Star screen awards,Global indian film awards na nyinginezo licha ya tuzo zote hizi kuwa za filamu lakini zote zinatoa tuzo ya best film,best actor, best actress,best director, best suporting actor/actress na nyingine kibao zikifanana lakini tuzo hizi zinztofautiana ubora na hata namna zinavyotolewa bali categories nyingi ni zile zile. hii ni kwa kuwa nchi hizi zina sera nzuri za kukuza sanaa ila BASATA inakuwa huzuni kama si kichekesho!. Hivi sera nzuri za sanaa lazima zipiganiwe na wasanii wakati hili tatizo linaonekana wazi wazi au BASATA huwa hawatazami tuzo za wasanii wa nje zinapotolewa, mbona kwenye media washindi wa tuzo za wenzetu wanatolewa kila siku!.Hii ndiyo maana tuzo za kilimanjaro Music Awards licha ya kulalamikiwa miaka nenda rudi kwa mapungufu mengi lakini kama ziko vile vile miaka yote kwa kuwa hakuna tuzo nyingine za za kutoa changamoto kama kwa wenzetu. hivi mwandaaji wa tuzo ni msanii kiasili?.
Tatizo jingine linalolalamikiwa na wadau ni kiasi kikubwa cha pesa zinazotozwa na BASATA 1,705,000 ili mtu apate kibali cha kuandaa tuzo. Hivi BASATA imeshindwa kujiuliza ni kwanini miaka kadhaa sasa imepita tangu tuzo za filamu za Vinara Awards kufanyika na mpaka leo hazijafanyika tena. Haijui kuwa sababu ni gharama za kuendesha tuzo na wadhamini kutokujitokeza. kwanini mpaka leo haiulizi au kushangaa kwa tuzo hizo kutofanyika tena kama kweli ipo kwa ajili ya kukuza sanaa maana ikumbukwe kuwa tuzo zile zilileta hamasa kubwa sana kwa wasanii kufanya kazi zenye viwango na kwa bidii.Tuzo ni sehemu ya kuchochea sanaa ikue na iwe na ushindani kwa kuwa kila mtu anafanya kazi bora ili azawadiwe na kutambulika kwa kazi nzuri, tuzo pia ni sehemu ya kuwa-promote wasanii mpaka nje ya nchi lakini ziko wapo tuzo za sanaa Tanzania! . Tena basi niseme wazi kuwa licha ya BASATA kutakiwa kufanya mabadiliko ya sera ya sanaa haraka kabla wadau hawajachachamaa ili sera ya sanaa ibadilike na kuruhusu tuzo mbalimbali , BASATA yenyewe inatakiwa iige mfano wa Serekali ya India kuwa na tuzo zake za kuwatukuza wasanii waliofanya vizuri kila mwaka,tuzo za National Awards zinazofanyika kila mwaka Bollywood zinasimamiwa kwa kila kitu na serikali ya India zikichuana na tuzo nyingine kubwa kila mwaka katika kuwazawadia wasanii bora. BASATA inazo hizo tuzo za kuwapongeza wasanii wa kada mbali mbali kila mwaka!.
Kwa kumalizia ni kuwa tatizo la kutokuwepo kwa tuzo za filamu na hata katika sanaa nyingine ili kuleta ushindani linasababishwa na sera mbovu ya sanaa nchini na bila kupiganiwa na wasanii ili kupata sera nzuri BASATA bado itaendelea kulinda sera hii ili "kukuza" sanaa nchini. Ni ukweli usiopingika kuwa leo hii tuzo mbalimbali za filamu au muziki zikianzishwa sanaa yetu itakuwa haraka na kuleta ushindani mkubwa sana kwa mataifa mengine kwa kuwa wasanii wetu watakuwa na ari ya kufanya kazi zilizo bora zaidi ili mwisho wa siku mtu aonekane yeye ndiye bora. BASATA inatakiwa itambue sasa kuwa nchi zote zilizoendelea katika sanaa hizi zina sera nzuri za sanaa kiasi cha kuruhsu tuzo kibao ili kuleta ushindani wa kukuza sanaa na siyo mtu mmoja kusajiliwa kwa kuandaa tuzo halafu eti yeye ndiye anakuza sanaa hivi wasanii wakigoma kutaka tuzo mbalimbali yeye atakuza sanaa gani!. kwa leo niishie hapa ila wadau tutoe maoni mbalimbali hii ni kwa kuwa maoni hutofautiana. Ahsanteni

No comments:

Post a Comment